**************************
Na Ahmed Mahmoud,Arusha
Serikali ya Tanzania imemuonya vikali mtu
anayejiita Nabii Namba saba ambaye jina lake halisi ni Mosses Mollel
kuwa itamchukulia hatua kali iwapo atashindwa kuthibitisha madai kuwa
na uwezo wa kutibu virusi Vya ugonjwa wa Corona .
Nabii huyo ambaye
taarifa zake zilianza kusambaa mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia
mitandao mbalimbali ya kijamii akidai anayodawa ya kutibu ugonjwa hatari
wa Corona ulioanzia nchini China na kusababisha Vifo Vya watu zaidi ya
1100 hadi sasa,ametakiwa kujisalimisha wizara ya afya na kuthibitisha
taarifa hizo.
Akiongea na Vyombo
Vya Habari jijini Arusha,Naibu Waziri wa Afya,Dkt Faustine Ndugulile
ameeleza kuwa anazo taarifa za Nabii huyo kujitangaza kuwa anayodawa ya
kutibu ugonjwa huo na kumtaka athibitishe kauli yake
“Kimsingi nimeiona
hiyo taarifa ya huyo mtu anayejiita Nabii Saba kuwa anayo dawa ya
kutibu ugonjwa wa Corona ,ila hapa kwetu Tanzania hatuna maambukizi
yoyote ya ugonjwa huyo ,tunachotaka huyo mtu atuthibitishie uwezo wake
wa kutibu huyo ugonjwa wa Corona” Amesema Ndugulile
Ameongeza kuwa iwapo atashindwa kuthibitisha atachukuliwa hatua Kali za kisheria.
Amesema hadi sasa
Serikali imetuma wataalamu wake kwenda kumsaka na kumhoji kama anavyo
vibali Vya kutoa huduma ya Tiba na kujitangaza kuwa anatoa Huduma ya
kutibu ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa mataifa bado yanahaha kusaka
Tiba ya ugonjwa huo.
Nabii Namba Saba
ambaye ni mkazi wa Ngaramtoni Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha amekuwa
akijitangaza kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo wa corona na kuweka
mawasiliano yake kwenye mitandao .
“Ninayodawa hapa Arusha ya kutibu virusi Vya Corona inayowaua Wachina na mataifa mengine. ” sauti ya Nabii huyo.
No comments :
Post a Comment