Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) akijibu maswali ya wabunge
wakati wa Bunge la kumi na nane Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020.
Sehemu
ya mawaziri akiwemo Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb), Waziri wa
TAMISEM Mhe Suleima Jaffo na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi
Mhandisi Hamad Masauni wakifatilia kipindi cha maswali na majibu akijibu
maswali ya wabunge wakati wa BUnge la kumi na nane Jijini Dodoma tarehe
6 Februari 2020.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) akijibu maswali ya wabunge
wakati wa BUnge la kumi na nane Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020.
MHE HUSEIN BASHE, NAIBU WAZIRI WA KILIMO AKIJIB…
MAREKEBISHO YA SHERIA YA VYAMA VYA USHIRIKA KUTUA BUNGENI-MHE BASHE
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein
Bashe (Mb) akijibu maswali ya wabunge wakati wa
Bunge la kumi na nane
Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020.
Sehemu ya mawaziri akiwemo Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb), Waziri wa TAMISEM Mhe Suleima Jaffo
na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni
wakifatilia kipindi cha maswali na majibu akijibu maswali ya wabunge
wakati wa BUnge la kumi na nane Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein
Bashe (Mb) akijibu maswali ya wabunge wakati wa BUnge la kumi na nane
Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Wizara ya Kilimo ipo katika hatua
za mwisho kupeleka Bungeni mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya
Maendeleo ya Ushirika yatakayoendana na mahitaji ya sasa ambayo
yatahusisha mabadiliko ya mfumo na muundo wa uongozi ili kuendana na
mahitaji ya teknolojia na kuleta ushindani wa kibiashara.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein
Bashe (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020
wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Mbinga vijijini Mhe Martini
Mtonda Msuha aliyetaka kufahamu serikali ina mpango gani wa kurekebisha
Sheria ya Vyama vya ushirika ili kuondoa mapungufu yaliyopo, hususani
kwa upande wa uanachama na kuipa serikali nguvu za kisheria juu ya Vyama
vya ushirika.
Bashe amesema kuwa Ilani ya
uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2015 – 2020 (Ibara ya 22 (g)(iv) na 86
(a) inaelekeza “Kuifanyia mapitio Sera ya Vyama vya Ushirika na
kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na upatikanaji wa
takwimu zitakazosaidia kuandaa mipango na kuleta mageuzi katika Sekta ya
Ushirika na kuimarisha uchumi wa Taifa na Kuviimarisha vyama vya
ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ya ndani
na nje kwa kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na uenezaji
wa taarifa za masoko na kutoa elimu juu ya uongezaji thamani na
biashara“
Amesema kuwa Ushirika ni dhana ya
hiari, lakini Serikali ni msimamizi mkuu wa vyama vya ushirika pale
ambapo viongozi wake au vyama vyenyewe havitekelezi malengo
yaliyokusudiwa na dhamira ya kuanzishwa kwa sekta ya ushirika.
Serikali inakiri vyama
vinakabiliwa na changamoto za kiutendaji, usimamizi, viongozi kutokuwa
waadilifu na mapungufu ya kimfumo ya uendeshaji wa vyama vya Ushirika
hapa nchini.
Hata hivyo, Bashe amesema vipo
baadhi ya vyama vya ushirika ambavyo vinafanya vizuri. Mfano, Chama cha
Ushirika cha Chai Mkonge, Mafinga na Chama Kikuu cha Ushirika Kahama
(KACU).
Kadhalika Mhe Bashe ameongeza kuwa
Ushirika ndicho chombo cha kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi kwa
kuwaunganisha wakulima ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kutoa huduma
za ugani, upatikanaji wa pembejeo na kutafuta masoko ya mazao.
MWISHO
CODES…!
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
*******************************
Wizara ya Kilimo ipo katika hatua za
mwisho kupeleka Bungeni mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya
Maendeleo ya Ushirika yatakayoendana na mahitaji ya sasa ambayo
yatahusisha mabadiliko ya mfumo na muundo wa uongozi ili kuendana na
mahitaji ya teknolojia na kuleta ushindani wa kibiashara.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein
Bashe (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020
wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Mbinga vijijini Mhe Martini
Mtonda Msuha aliyetaka kufahamu serikali ina mpango gani wa kurekebisha
Sheria ya Vyama vya ushirika ili kuondoa mapungufu yaliyopo, hususani
kwa upande wa uanachama na kuipa serikali nguvu za kisheria juu ya Vyama
vya ushirika.
Bashe amesema kuwa Ilani ya uchaguzi
ya Chama cha Mapinduzi 2015 – 2020 (Ibara ya 22 (g)(iv) na 86 (a)
inaelekeza “Kuifanyia mapitio Sera ya Vyama vya Ushirika na kusimamia
utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na upatikanaji wa takwimu
zitakazosaidia kuandaa mipango na kuleta mageuzi katika Sekta ya
Ushirika na kuimarisha uchumi wa Taifa na Kuviimarisha vyama vya
ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ya ndani
na nje kwa kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na uenezaji
wa taarifa za masoko na kutoa elimu juu ya uongezaji thamani na
biashara“
Amesema kuwa Ushirika ni dhana ya
hiari, lakini Serikali ni msimamizi mkuu wa vyama vya ushirika pale
ambapo viongozi wake au vyama vyenyewe havitekelezi malengo
yaliyokusudiwa na dhamira ya kuanzishwa kwa sekta ya ushirika.
Serikali inakiri vyama vinakabiliwa
na changamoto za kiutendaji, usimamizi, viongozi kutokuwa waadilifu na
mapungufu ya kimfumo ya uendeshaji wa vyama vya Ushirika hapa nchini.
Hata hivyo, Bashe amesema vipo
baadhi ya vyama vya ushirika ambavyo vinafanya vizuri. Mfano, Chama cha
Ushirika cha Chai Mkonge, Mafinga na Chama Kikuu cha Ushirika Kahama
(KACU).
Kadhalika Mhe Bashe ameongeza kuwa
Ushirika ndicho chombo cha kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi kwa
kuwaunganisha wakulima ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kutoa huduma
za ugani, upatikanaji wa pembejeo na kutafuta masoko ya mazao
No comments :
Post a Comment