Baadhi ya vitu vya asili kutoka
Makunduchi,ukiwemo Msikiti Kichaka, vyakula na kupigana magomba,
vilifanywa katika Tamasha la Utalii wa ndani kwa kutumia Baskeli Mkoa wa
Kusini Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja
Ayoub Mohamed Mahmoud wa kwanza (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa
mwakakogwa Mzee Mwita wakati wakiwa katika ziara ya Tamasha la Utalii wa
Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja.
Mmoja wa Washiriki wa Tamasha la
Utalii wa Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja Kudrat Mussa kutoka Tanzania
Bara akikabidhiwa Cheti cha ushiriki wa Tamasha hilo na Mkuu wa Mkoa wa
Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Kiboje Wilaya ya kati.
Fundi Mkuu wa Baskeli katika
msafara wa Tamasha la Utalii wa Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja Juma
Lukodwa akikabidhiwa Cheti cha ushiriki wa Tamasha hilo na Mkuu wa Mkoa
wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Kiboje Wilaya ya kati.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja
Ayoub Mohamed Mahmoud akimkabidhi Cheti cha ushiriki wa Tamasha la
Utalii wa ndani kwa kutumia Baskeli Vuai Ali Maneno kutoka Vilabu vya
Baskeli Zanzibar hafla iliyofanyika Kiboje Mkoa wa Kusini Unguja
Sheha wa Shehia ya Cheju Bitatu
akikabidhiwa Cheti cha ushiriki wa Tamasha la Utalii wa Baskeli na Mkuu
wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud katika Ufungaji wa
Tamasha hilo huko Kiboje Wilaya ya Kati.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja
Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi Baraza la Vijana la Wilaya ya kati
Baskeli na Vifaa vya kazi huko Kiboje Wilaya ya kati katika Ufungaji wa
Tamasha la Utalii wa ndani kwa kutumia Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja.

Baraza la Vijana
kutoka Wilaya ya Kusini Unguja wakikabidhiwa Baskeli na Vifaa vya kazi
na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud hafla
iliyofanyika Kiboje Wilaya ya kati.
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………………………………….
Na Mwashungi Tahir Maelezo
Mkuu wa Mkoa wa
Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud ameitaka jamii kutembelea vivutio
vya utalii ili kuelewa vivutio vya kitalii viliopo Zanzibar na kuachana
na dhana ya
utalii kwa wageni .
Akizungumza hayo
na Washiriki wa Tamasha la Utalii wa Baiskeli huko Shehia ya Kiboje
Mkoa wa Kusini Unguja wakati alipokuwa akifunga tamasha hilo na kuitaka
jamii , vijana kutembelea sehemu zenye mambo mbalimbali katika Mkoa huo.
Amesema
Wazanzibar wengi wanahisi utalii uko sehemu ya Forodhani , na kuwataka
waachana na dhana hiyo, kwa kufahamu kwamba utalii uko Zanzibar nzima
na una sehemu nyingi za vivutio takribani vingi sana ikiwemo Mkoa wa
Kusini Unguja.
“Watalii wengi
wanaona utalii upo Forodhani tu, hapana, utalii uko Zanzibar Nzima na
kuna vivutio vingi katika sehemu mbali mbali za Zanzibar”, Alisema Mkuu
wa Mkoa huyo.
Hata hivyo
amesema wazaliwa wa Nchi hii wawe wa mwanzo katika kukuza utalii wa
ndani na kuutangaza Utalii kwa wote na ili uwe endelevu kwa lengo la
kuuimarisha.
Aidha aliwataka
Wazanzibar kuweka mashirikiano na umoja kwa lengo la kuuweka utalii wa
ndani na utalii kwa wote katika Mkoa huo.
Pia alisema
katika Mkoa wa Kusini Unguja tushatekeleza kwa vitendo dhana hiyo ya
Utalii kwa kufanya matembezi katika maeneo mbali mbali ya kitalii yenye
vivutio vyote vya Kitalii na kuwapatia fursa vijana kuweza kujua mambo
yaliyomo .
Nae Mkuu wa
Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Kitwana Mustafa amesema rasilimali
zilizopo ndani ya Mkoa huo zitawafanya vijana kuzitumia kwa kupitia
ujasiriamali na mambo mengine ya kujiendeleza kwa kupitia vivutio hivyo
vya utalii.
Kwa upande wake
Mkuu wa Wilaya ya Kati Hamida Mussa Khamis amesema lengo kuu la
Tamasha hilo ni kuunga mkono Jitihada za Serikali ya Mapinduzi katika
Sekta ya Utalii wa ndani na Utalii kwa wote kwa kufanya kwa vitendo.
Pia amesema ndani ya tamasha hilo vijana wameweza kujifunza na kuelimika kwa mambo mengi ambayo walikuwa hawayajui.
Nao washiriki wamevutika sana kwa matembezi hayo na kuahidi mwakani watajitokeza zaidi.
Zaidi ya vivutio
vya utalii wa ndani na Utalii kwa wote 13 vimeweza kutembelewa na
washiriki kukabidhiwa vyeti na Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tena
ifikapo Ijumaa ya mwisho January 2021 ndani ya Mkoa huo
No comments :
Post a Comment