Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani akiwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu kwenye wa hafla ya kukabidhi cheti cha
Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa bomba la kusafirisha
mafuta ghafi la Afrika Mashariki(EACOP)iliyofanyika katika ofisi za
Makamu wa Rais iliyopo Mtumba mjini Dodoma.
Mratibu wa Mradi wa EACOP kutoka
Wizara ya Nishati, Salum Mnuna(wa kwanza kulia) Kamishna wa Nishati na
Gesi Adam Zuber na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha
mafuta ghafi Martin Tiffen akiwa kwenye wa hafla ya kukabidhi cheti cha
Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa bomba la kusafirisha
mafuta ghafi la Afrika Mashariki(EACOP)iliyofanyika katika ofisi za
Makamu wa Rais iliyopo Mtumba mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza katika wa
hafla ya kukabidhi cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi
wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika
Mashariki(EACOP)iliyofanyika katika ofisi za Makamu wa Rais iliyopo
Mtumba mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza wa hafla ya kukabidhi cheti
cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa bomba la kusafirisha
mafuta ghafi la Afrika Mashariki(EACOP)iliyofanyika katika ofisi za
Makamu wa Rais iliyopo Mtumba mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa
la Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka akimkabidhi cheti
cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa bomba la kusafirisha
mafuta ghafi la Afrika Mashariki(EACOP) Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa
bomba la kusafirishia mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda mpaka Tanga
Tanzania, Martin Tiffen .
Viongozi mbalimbali kutoka Wizara
ya Nishati na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano pamoja na
Menejimenti ya Mradi wa EACOP akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
makabidhiano ya cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa
bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika
Mashariki(EACOP)yaliyofanyika katika ofisi za Makamu wa Rais iliyopo
Mtumba mjini Dodoma.
………………………………………………………………………………………………………..
Hafsa Omar-Dodoma
Waziri wa
Nishati, Dkt Medard Kalemani amesema kuwa ujenzi wa Mradi wa Bomba
la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka...
Hoima Uganda mpaka Tanga
nchini Tanzania( EACOP) unaendelea kutekelezwa kama ulivyopangwa na
hautarudi nyuma na tayari nchi zote mbili zipo kwenye hatua za
utekelezaji.
Ameyasema hayo,
Februari 6,2020 wakati wa hafla ya kukabidhi cheti cha Tathmini ya
Athari kwa Mazingira kwa Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la
Afrika Mashariki(EACOP)iliyofanyika katika ofisi za Makamu wa Rais
iliyopo Mtumba mjini Dodoma.
Aidha, alieleza
kuwa tayari hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa na Serikali ya
Tanzania ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kama ulivyopangwa, hatua
hizo ni pamoja na kupata eneo ambalo litatumika kuwekea matenki makubwa
manne ya mafuta katika kata ya Chongoleani Mkoani Tanga.
Hatua nyingine
mbazo Serikali imezichukua ni upatikanaji wa korido ambayo ni njia ya
kupitishia bomba yenye kilomita 1414 kwa upande wa Tanzania na kwa
ujumla wake zitakuwa 1443 zikijumlishwa na kilomita 300 za upande wa
nchi ya Uganda.
Aliongeza kuwa,
hatua nyengine ambayo Serikali imechukua ni ukamilishaji wa kufanya
kazi ya tathmini ya fidia kwa wale wote ambao watakaopisha eneo la
korido hilo ambalo litapita katika wilaya zaidi ya 24 kata 86 na
vitongoji 278.
Aliendelea
kueleza kuwa, kazi ambazo kwasasa Serikali inazifanya ni pamoja na
majadiliaona baina ya nchi mbili husika kuhusu manufaa halisi ya
kiuchumi na kijamii katika nchi zote mbili, ambapo ajira zaidi ya 5000
zitapatikana kutokana na mradi huo ajira hizo ni pamoja na ajira za
kudumu na ambazo sio za kudumu.
Alisema kuwa,
ujenzi wa mradi huo utaanza rasmi mara tu baada ya majadiliano na
matayarisho hayo yatakapomalizika na ujenzi wa mradi huo utachukua
takribani zaidi ya miezi 36.
Vilevile, amesema
jambo hilo la makabidhiano ya cheti cha tathmini lilikuwa likisubiriwa
kwa muda mrefu na kwasasa limefungua fursa ya kuanza kwenda kwenye
hatua ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa na kuwataka wataalamu husika
wa mradi kila mtu katika nafasi yake kuanza kutekeleza wa mambo
mengine.
Kwa upande
wake, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira . Mhe. Mussa Azzan Zungu alisema kuwa hafla hiyo ya
kukabidhi Cheti cha Tathmini ya Mazingira kwa Mradi wa EACOP, ni
Ushahidi wa Serikali kuridhia kuwa Mradi huu utahakikisha kwamba masuala
ya kiuchumi, kijamii,mazingira,afya na usalama yanashughulikiwa wakati
wote wa kipindi cha kupanga, kujenga na uendeshaji wa shughuli za bomba
ili kupunguza athari kwa mazingira.
Pia,alisema mradi
huo wa bomba umezingatia maeneo muhimu ya kimazingira kama vile mbuga
za wanyama, Maeneo tengefu kama vile hifadhizi za misitu na maeneo yenye
idadi kubwa ya watu.
Aliongeza kusema
kuwa, vituo vitawekwa na kuendeshwa kwa umakini ili kupunguza athari
yoyote ya kimazingira na kiikolojia wakati wa utekelezaji wa Mradi huu
ambao unahitaji ushirikiano baina ya pande tatu Serikali mbili za
Tanzania na Uganda pamoja na Wawekezaji.
Aidha, alisema
kazi ya Serikali kupitia NEMC haiishii kutoa Cheti tu, bali kuendelea
kufuatilia na kutathmini utekelezaji wake kulingana na masharti ya Cheti
kilichotolewa.
“ Timu yangu
imejipanga na itaendelea kushirikiana na Wizara ya Nishati ambao ni
Msimamizi na Mratibu wa Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania pamoja na
wawekezaji pindi watakapoanza kutekeleza Mradi huu kwenye hatua ya
ujenzi na uendeshaji ili kuhakikisha kwamba mradi unatekelezwa kwa
kuzingatia hifadhi ya mazingira.”alisema.
Hafla hiyo pia
ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na Menejimenti ya Mradi wa
EACOP.
No comments :
Post a Comment