NA ANDREW CHALE
SERIKALI ya awamu ya tano
inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imedhamiria kwa dhati kuboresha Sekta ya
Afya
nchini na tayari imeleta mitambo ya kisasa ya Maabara ya upasuaji wa
Ubongo bila kufungua fuvu (Angio Suite).
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Mifupa (MOI), Patrick Mvungi ameeleza kuwa mitambo hiyo
imewasili Nchini ikitokea Ujerumani ambapo ni juhudi za Serikali ya
kuona wanasogeza huduma za kibingwa hapa nchini.
“Mitambo ya Maabara ya upasuaji wa Ubongo bila kufungua fuvu (Angio Suite) imewasili bandari ya Dar es salaam.
Mitambo, Vifaa vingine pamoja na
ukarabati wa Chumba vimegharamiwa na Serikali kwa gharama ya Tsh Bilioni
7.9.” Alisema mkuu wa kitengo cha Uhusiano MOI, Patrick Mvungi.
Na kuongeza kuwa ujio wa mitambo
hiyo ya upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu itakuwa msaada mkubwa kwa
wananchi na mataifa mengine hapa Barani Afrika wanaofika MOI kwa ajili
ya matibabu.
“Taasisi ya Mifupa-MOI pia tunatoa huduma mbalimbali za kibingwa na kibobezi zikiwemo;
Upasuaji wa Kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye Ubongo,
Upasuaji wa Mgongo kwa kufungua eneo dogo.
Upasuaji wa Kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye Ubongo,
Upasuaji wa Mgongo kwa kufungua eneo dogo.
Zipo pia huduma za Upasuaji wa
magoti kwa njia ya matundu, Upasuaji wa kupandikiza nyonga bandia,
Upasuaji wa kupandikiza goti bandia na Upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye
ubongo alieleza Mkuu wa kitengo cha Uhusiano MOI, Patrick Mvungi.
Huduma hizo na nyingine katika
taasisi hiyo zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi na mataifa mengine
barani Afrika ambapo awali walikuwa wakizifuata nje ya Nchi.
No comments :
Post a Comment