Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo (wa pili kulia) akiwasili ofisi za
Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma jana na kupokewa na viongozi
pamoja na watumishi wa Wizara hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu
ateuliwa katika nafasi hiyo.Wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu Nicolaus
Benjamin.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo akisalimiana na Mthamini Mkuu wa
Serikali Evalyne Mugasha alipowasili ofisi za Wizara eneo la Mtumba
jijini Dodoma jana ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ateuliwa katika
nafasi hiyo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisalimiana na Katibu Mkuu
Wizara hiyo Mary Makondo alipowasili ofisi za Wizara ya Ardhi eneo la
Mtumba jijini Dodoma jana ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ateuliwa
kushika nafasi hiyo.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Mary Makondo (Hayupo pichani) alipowasili ofisi za Wizara ya Ardhi
eneo la Mtumba jijini Dodoma jana ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu
ateuliwa kushika nafasi hiyo.
(PICHA NA HASSAN MABUYE WIZARA YA ARDHI)
……………………………………………………………………………………………………….
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo amewataka
watumishi wa sekta ya ardhi katika Wizara hiyo kushirikiana ili
kuibadilisha
Wizara na kuwa na utendaji bora utakaokidhi mahitaji ya
wananchi.
Makondo alisema
hayo jana wakati akizungumza na watumishi wa wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi alipowasili kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kushika
wadhifa huo.
Makondo alichukua
nafasi hiyo kutoka kwa Dorothy Mwanyika aliyestaafu kwa mujibu wa
Sheria. Kabla ya Uteuzi huo Makondo alikuwa Kamishna wa Ardhi kwenye
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Alisema,
mategemeo ya watumishi wa Wizara ya Ardhi mara baada ya kuteuliwa kwake
ni makubwa lakini msisitizo wake ni watumishi hao kufanya kazi kwa bidii
na kwa kujituma ili kuweza kuibadilisha Wizara.
‘’Kauli ya Wizara kuwa ina ‘madudu’ siyo nzuri hivyo tukimbie ili tuwe na sekta ya ardhi iliyobadilika’’ alisema Makondo.
Katibu Mkuu huyo
wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitaka kuthaminiwa kwa
mchango wa kila mtumishi wa Wizara hiyo kwa kuwa ndiyo njia pekee
itakayoleta mabadiliko na mafanikio ya utendaji kazi wa sekta hiyo.
Kwa mujibu wa
Makondo, Kampuni ya utengenezaji magari ya Toyota imefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kwenye biashara zake kutokana na kutumia mfumo wa Kaizen
unaothamini mchango wa kila mmoja katika utendaji kazi.
Makondo amewataka
pia watumishi wa Wizara ya Ardhi kuweka miakakati ya pamoja kwa lengo
la kuibadilisha wizara hapo ilipo ili kuonesha kuwa wizara hiyo
imebadilika katika utendaji wake.
Baadhi ya
Watumishi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi walioneshwa
kufurahishwa na uteuzi wa Katibu Mkuu huyo kwa kuwa ametokea Wizara hiyo
na anaijua sekta ya ardhi vizuri pamoja na watumishi wake.
No comments :
Post a Comment