**********************************
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema hadi Desema 2019, ujenzi wa reli ya kati ya
kisasa (Standard Gauge) kwa sehemu ya Dar es Salaam – Morogoro (kilometa
300) umefikia
asilimia 70.
Amesema hatua
hiyo ni miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa
Bajeti ya Serikali iliyopitishwa na Bunge kwa kipindi cha kuanzia Julai
hadi Desemba, 2019.
Waziri Mkuu
ameyasema hayo leo (Ijumaa, Februari 7, 2020) wakati akiahirisha mkutano
wa 18 wa Bunge la 11 bungeni jijini Dodoma. Amesema mafanikio hayo
yametokana na kuimarika kwa mapato.
Amesema kazi
za ujenzi kwa sehemu ya Morogoro – Makutupora (kilometa 422) zinaendelea
vizuri na Serikali imerejesha huduma ya reli ya abiria na mizigo ya
Kaskazini (Dar es Salaam – Moshi).
Waziri Mkuu
ametaja mafanikio mengine kuwa ni kuendelea na ujenzi wa Mradi wa kufua
Umeme wa Maji wa Julius Nyerere ambapo kazi zilizokamilika ni pamoja na
ujenzi wa daraja la muda namba 2; utafiti wa miamba na udongo; uchimbaji
wa mtaro wa chini kwa chini wenye urefu wa mita 147.6.
Pia, Waziri
Mkuu amesema Serikali imefanikiwa kuendeleza Mradi wa Usambazaji Umeme
Vijijini (REA) ambapo hadi Desemba 2019 jumla ya vijiji 8,236 kati ya
vijiji 12,268 vya Tanzania Bara vimeunganishwa na umeme, sawa na
asilimia 67.1.
“Aidha,
kufuatia malalamiko ya ucheleweshaji wa baadhi ya miradi ya REA,
namuagiza Waziri wa Nishati kuhakikisha wakandarasi wote kwenye mpango
wa REA wanakamilisha majukumu yao kwa wakati,” amesema.
Kuhusu
usafiri wa anga, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuboresha
Shirika la Ndege Tanzania kwa kununua ndege mpya 11. “Hadi Desemba 2019,
ndege 8 zimepokelewa na malipo ya awali ya ununuzi wa ndege nyingine
mpya tatu yameshafanyika.”
“Kuzinduliwa
kwa Jengo la Tatu la abiria katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere na kuanza kutumika kuhudumia abiria; kuendelea na
uboreshaji wa kiwanja cha ndege Mwanza na viwanja vya mikoa mbalimbali.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara kwa
kiwango cha lami zikiwemo barabara kuu, barabara za mikoa na za wilaya.
Mtandao wa barabara kuu umefikia kilometa 8,502 na mtandao wa barabara
za mikoa kilometa 1,756.
Pia, Serikali imeendelea na ujenzi wa Ubungo inter-changeambapo
hadi Desemba 2019 ulifikia asilimia 62 na ujenzi wa barabara ya njia
nane kutoka Kimara hadi Kibaha umefikia asilimia 63.
Kuhusu
miundombinu ya madaraja Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea
kukamilisha ujenzi wa madaraja ya Sibiti (Singida), Momba (mpakani mwa
Songwe na Rukwa), Mlalakuwa (Dar es Salaam), Lukuledi (Lindi) na
kuendelea na ujenzi wa daraja la Selander na daraja la Kigongo – Busisi
lenye urefu wa mita 3,200 na upana wa mita 28.45.
“Mbali na
hayo tunaendelea na ujenzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria
1,200 na tani 400 za mizigo katika Ziwa Victoria ambapo utekelezaji wake
umefikia asilimia 37; ujenzi wa chelezo umefikia asilimia 46; ukarabati
wa meli ya MV Victoria umefikia asilimia 65 na MV Butiama asilimia 60.”
Amesema hatua
nyingine inayochukuliwa na Serikali ni kukamilika kwa ujenzi wa kivuko
kipya cha Kigongo – Busisi; kuendelea na ujenzi wa kivuko kipya cha
Nyamisati – Mafia; kuendelea kukarabati vivuko vya MV Sengerema
(asilimia 40); MV Kigamboni (asilimia 60), na MV Utete (asilimia 95).
Akizungumzia
kuhusu bandari ya Dar es Salaam, Waziri Mkuu amesema upanuzi wa bandari
hiyo unaendelea ambapo ujenzi wa gati namba moja, mbili na tatu pamoja
na gati la kupakia na kupakua magari (Ro-Ro) umekamilika.
Waziri Mkuu
amesema kukamilika huko kwa gati la kupakia na kupakua magari
kutawezesha meli ya kwanza yenye uwezo wa kubeba magari 6,000 kuhudumiwa
katika gati hilo. Uboreshaji wa bandari za Tanga, Mtwara na bandari za
maziwa makuu pia unaendelea.
No comments :
Post a Comment