******************
Na Magreth Kinabo- Mahakama
Jaji Mkuu wa
Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma amesema ipo haja ya kutoa
taarifa fupi kuhusu kesi zenye mvuto katika jamii ili ziweze kueleweka
kwa umma.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Majaji wa Mahakama ya Tanzania na
Majaji wa Mahakama ya Uingereza lililoanza Februari 3 na linatarajia
kumalizika Februari 4, mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu
J.K . uliopo jijini Dar es Salaam, Jaji Mkuu alisema majaji ya Uingereza
wao tayari wanafanya hivyo.
‘‘Itabidi
tubadilike sisi Majaji huenda pale tunadhani kesi zenye mvuto katika
jamii, tuanze na sisi kutoa taarifa fupi , ikiwemo kuandika hukumu ili
ujumbe uweze kufika kwa wananchi, alisema Jaji Mkuu.
Alisema kesi hizo
zinapaswa kutolewa kwa taarifa hiyo zikiwa katika nakala ngumu na laini
sambamba na lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
Aidha Jaji Mkuu
akizungumzia kuhusu kongamano hilo, alisema lina lengo la kushifrikiana
na kubadilishana uzoefu kwa kuwa taratibu mbalimbali za kimahakama baina
nchi hizo mbili zinafanana.
Aliongeza kuwa kupitia ushirikiano huo, tayari Majaji 21 na Mahakimu 24 wamepatiwa mafunzo.
Hivyo kupitia
ushirikiano huo, utasaidia kuleta matokeo chanya katika maboresho
yanayoendelea kwenye Mahakama ya Tanzania na ukiwemo Mpango Mkakati wa
Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania, kuanzia mwaka 2015/16 hadi
2019/20.
Kwa upande wake,
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi
alisema Mahakama inafanya kazi na nchi zote zilizopo katika Jumuia ya
Madola ili kuweza kuboresha utendaji kazi na kuweza kuwa na mifumo
bora na kiwango kinachokubalika..
Hivyo kongamano
hilo ni fursa litasaidia kuongeza ujuzi kwa Majaji wa Tanzania kuweza
kutoa maamuzi hasa katika kesi kubwa za wawekezaji kutoka nje ya nchi..
Dkt. alisema nchi
inaongezeka kuwa na wawekezaji wengi wa kigeni , hata katika mahakama
zetu kuna mashauri yanayofunguliwa na kampuni za kigeni.
No comments :
Post a Comment