Friday, February 21, 2020

HOSPITALI YA BUGANDO YASHIRIKI MAONESHO KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MADAKTARI TANZANIA


Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando,Leo Februari 20, 2020 imeshiriki katika Maadhmisho ya siku ya madaktari Tanzania,kwa kufanya maonyesho ya huduma inazozitoa. katika mkutano huo ambao
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amezungumza na madaktari,  akizungumza katika  SIKU YA MADAKTARI TANZANIA ametoa Rais ametoa agizo kwa viongozi wa TAMISEMI na Wizara ya Afya kukutana na kutatua changamoto zinazowakabili madaktari.
“Natoa agizo kwa viongozi wa TAMISEMI na Wizara ya Afya kushughulikia changamoto zote zilizotolewa na Madaktari kwani changamoto hizo zikitatuliwa zitasaidia kuboresha sekta ya afya” Amesema Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Pamoja na hayo amesema, Sekta ya afya ni muhimu kwa ustawi na maendeleo ya taifa lolote hasa katika kukuza uchumi, endapo nchi za Afrika zitaweza kupunguza na kutokomeza magonjwa tutakuza uchumi wetu hivyo kupunguza umaskini. wetu
Katibu wa Wizara ya Afya Bi Zainabu Chaula (kulia), akifurahia jambo huku  Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Prof. Abel Makubi (wa pili kutoka kulia ) na Dkt.Lucas Kiyeji – daktari bingwa wa magonjwa ya saratani Bugando (katikati ) wakimuangalia wakati alipotembelea katika banda la Hospitali ya Bugando siku Maadhimisho ya madaktari Tanzania Februari 20,2020
Katibu wa Wizara ya Afya Bi Zainabu Chaula akizungumza jambo huku Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Prof. Abel Makubi wa pili kutoka kulia  na Dkt.Lucas Kiyeji – Daktari bingwa wa magonjwa ya saratani Bugando ( katikati)  wakimsikiliza wakati alipotembelea katika banda la Hospitali ya Bugando siku Maadhimisho ya madaktari Tanzania Februari 20,2020
Katibu wa Wizara ya Afya Bi Zainabu Chaula akisalimiana na baadhi ya madaktari wa Bugando(Wa pili kutoka kulia), ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Prof. Abel Makubi na Dkt.Lucas Kiyeji – daktari bingwa wa magonjwa ya saratani Bugando ( katikati ) wakati alipotembelea katika banda la Hospitali ya Bugando siku Maadhimisho ya madaktari Tanzania Februari 20,2020

No comments :

Post a Comment