Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amefanya ziara ya kukagua ukarabati
wa miundombinu ya shule ya wasichana ya sekondari Msalato uliofanywa na
wizara katika shule hiyo pamoja na kuzungumza na wanafunzi wa hiyo.
Baada ya kukagua ukarabati huo
Waziri Ndalichako alizungumza na walimu, watumishi na wanafunzi wa shule
hiyo na kuwataka kuendelea na juhudi wanazozifanya katika kuhakikisha
shule hiuyo inakuwa na matokeo mazuri kama ilivyofanya kwa kipindi cha
miaka 10 mfululizo ya kuongeza ufaulu na kutopata daraja la sifuri
katika matokeo ya kidato cha nne.
“Nawapongeza kwa kuwa shule ya
wasichana yenye matokeo mazuri kwa kipindi kirefu, niwaombe ongezeni
bidii ili matokeo ya elimu bila malipo yaweze kuonekana kwani rais
anapambana kuhakikisha elimu inakuwa bora ikiwa ni pamoja na kuongeza
bajeti ya Elimu sekondari kwa asilimia 70 mwaka uliopita” amesisitiza
Profesa Ndalichako.
Waziri Ndalichako ameeleza kuwa
matokeo chanya ya Sera ya Elimu Bila Malipo ni kuongezeka wa wanafunzi
wanaomaliza darasa la saba na kutakiwa kujiunga na kidato cha kwanza,
ambapo ameeleza kuwa takwimu zinaonesha kuna ongezeko la wanafunzi hao
kutoka 366,296 mwaka 2016, kufikia 680,000 mwaka 2020, na inatarajiwa
Mwaka 2023 watakuwa 1,400,00 na hivyo kuhitajika kuongeza miundo mbinu
ya shule za sekondari kwa zaidi ya asilimia 100.

Ndalichako amesema ni katika
kuangalia hili Serikali ilikuja na Mradi wa Kuimarisha Elimu ya
Sekondari (SEQUIP) na kuomba ufadhili wa Benki ya Dunia. Ndalichako
amesema kuwa anaamini Benki ya Dunia itaridhia na kupitisha mradi huo
muhimu kwa taifa kwa sababu unakwenda kutatua mahitaji ya haraka ya
kielimu ya watoto wa Kitanzania na kutimiza Malengo Endelevu ya
maendeleo.
Waziri Ndalichako amefafanua kuwa
kuwa mradi huu una lenga kuongeza idadi ya shule za sekondari ambazo
zitajengwa katika maeneo karibu na jamii ili watoto wasoe katika
mazingira salama, kuongeza shule za bweni hususan kwa ajili ya watoto wa
kike, upanuzi wa shule kongwe 50 ili kuongeza nafasi na kukamilisha
maabara. Kimsingi, wanafunzi zaidi ya 6,000,000 wa kike na kiume
watanufaika na Mradi katika kipindi cha miaka 5 ijayo.

Mradi pia utawezesha uboreshaji wa
vituo vya utoaji elimu kwa Mfumo Mbadala kupitia vyuo vya Maendeleo ya
Wananchi (FDCs) na Vituo vya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (AEP)
Centers na ambao utawezesha wanafunzi awalioacha Shule kwa sababu
mbalimbali kupata elimu na kumuwezesha kurejea katika mfumo rasmi.
“ lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa kila mtoto wa kitanzania anapata elimu na katika
miaka miwili iliyopita tulifanya kazi kwa
pamoja na wadau na kuja na mfumo huu ”“ lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa kila mtoto wa kitanzania anapata elimu na katika
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Gerald
Mweli amesema TAMISEMI itaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknlojia kuhakikisha inakamilisha ukarabati wa shule kongwe
kwa kukarabati maeneo ambayo hayakufikiwa katika awamu ya kwanza huku
akipongeza juhudi za walimu wa shule hiyo kwa kuondoa daraja sifuri.
Mkuu wa shule Neema Maro
ameishukuru serikali kwa namna inavyokarabati shule kongwe ikiwa pamoja
na kuweka mazingira wezeshi ya ufundishaji na ujifunzaji, huku akiomba
kutatuliwa changamoto ya uzio, uchakavu wa baadhi ya miundombinu ambayo
bado haijakarabatiwa shuleni hapo.
No comments :
Post a Comment