Waziri wa Nishati, Dk. Medard
Kalemani,akizungumza na wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA awamu ya
tatu, watendaji wa REA pamoja na Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania
(TANESCO),wenye lengo la kujadili utekelezaji wa usambazaji umeme
vijijini mkutano huo umefanyika jijini Dodoma leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa
Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga,akizungumza wakati wa
kikao cha kujadili utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini jijini
Dodoma leo.
Sehemu ya washiriki wakifatilia
hotuba ya Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani,alipokuwa akizungumza
na wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA awamu ya tatu, watendaji wa
REA pamoja na Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO),kwa ajili
ya kujadili utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini kikao hicho
kimefanyika jijini Dodoma leo.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati, Mhandisi Leonard Masanja,akizungumza na wakandarasi
wanaotekeleza mradi wa REA awamu ya tatu, watendaji wa REA pamoja na
Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO),wenye lengo la kujadili
utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini kikao hicho kimehudhuriwa na
Waziri wa Nishati Dk.Kalemani jijini Dodoma leo.

Waziri wa Nishati, Dk. Medard
Kalemani,akisisitiza jambo alipokutana na wakandarasi wanaotekeleza
mradi wa REA awamu ya tatu, watendaji wa REA pamoja na Shirika la
Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO),wenye lengo la kujadili utekelezaji
wa usambazaji umeme vijijini mkutano huo umefanyika jijini Dodoma leo
kushoto kwake ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe.Subira Mgalu
PICHA ALEX SONNA-FULLSHANGWE BLOG
……………………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali
imewaagiza wakuu wa wilaya na mameneja wanaosimamia Mradi wa Usambazaji
Umeme Vijijini (REA) kuwakamata wakandarasi watakaoshindwa kutekeleza
mpango kazi wa
usambazaji umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa
kwanza.
Hayo ameyasema leo jijni Dodoma
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani,wakati alipokutana na
wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA awamu ya tatu, watendaji wa REA
pamoja na Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO), kujadili
utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini.
Waziri Kalemani amesema kuwa kila
mkandarasi anapaswa kuwasilisha mpango kazi kuonyesha majina ya vijiji
watakavyoenda kuwasha umeme kila na uwasilishe kwa wakuu wa wilaya.
Aidha Mhe.Kalemani amepiga
maarufuku wakandarasi kusimamisha nguo za umeme bila kuweka
nyaya,transform na kuwasha umeme kuanzia Februari 15 mwaka huu hatua za
kinidhamu zitachukuliwa kwa mkandarasi atakayesimamisha nguzo kwa zaidi
ya wiki moja bila kuwasha umeme.
”Hivyo nawaomba
wakuu wa wilaya na Mameneja wa TANESCO fatilieni kama kuna mkandarasi
husika anatekeleza mpango kazi wake kama alivyouwasilisha na achukue
hatua ya kuwakamata wakandarasi watakaoshindwa kutekeleza mpango kazi
wao”amesema Mhe Kalemani.
Waziri amsema
kuwa kuna baadhi ya maeneo ambayo wakandarasi wamesimamisha nguzo bila
kuweka nyaya, transfoma na kuwasha umeme, hivyo aliagiza mameneja
kusimamia wakandarasi wawashe umeme haraka.
Aidha amesema
kuwa malalamiko ya wakazi wa maeneo ya visiwani kuuziwa umeme kwa
gharama kubwa, ni marufuku kwa wananchi wa maeneo ya visiwani kuuziwa
umeme uniti moja kwa sh. 2500.
Dk.Kalemani amesema kuwa bei halali wanayopaswa kuuziwa umeme wananchi wa maeneo hayo ni sh. 100 kwa kila uniti moja.
“Nilipofanya
ziara Ukerewe na Mafia nimekuta malalamiko hayo na Sasa naelekeza wateja
wote wadogo ambao matumizi yao ya umeme ni chini ya uniti 75 kwa mwezi,
malipo yao ni sh. 100 kwa kila uniti moja,” amesema
Awali , Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga, amesema kuwa kumekuwa na
utekelezaji hafifu wa mradi wa REA awamu ya tatu, kuanzia Januari mwaka
huu.
Amesema kuwa
kuanzia Januari hadi sasa ni vijiji 54 pekee ndivyo vilivyounganishiwa
umeme, hivyo mkutano huo utatumika kubaini sababu za baadhi ya
wakandarasi kushindwa kutekeleza mradi kama ilivyopangwa.
No comments :
Post a Comment