
Baadhi ya Nyumba za Waathirika wa
Maafa ya Upepo Mkali na Mvua za masika zilizowekewa Jiwe la Msingi na
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt,Hussein Ali Mwinyi Nungwi Wilaya ya Kaskazini A
Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Hussein Ali Mwinyi
wapili kushoto akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni
ya kukabiliana na Maafa Makame Khatib Makame wakati akitembelea Nyumba
za Waathirika wa Maafa ya Upepo Mkali na Mvua za masika zinazofadhiliwa
na Shirika la Mwezi Mwekundu baada ya kuweka Jiwe la Msingi Nungwi
Wilaya ya Kaskazini A Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 56 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Hussein Ali Mwinyi
wakwanza kushoto akikunjuwa kitambaa ikiwa ni ishara ya Kuweka Jiwe la
Msingi Nyumba za Waathirika wa Maafa ya Upepo Mkali na Mvua za masika
zinazofadhiliwa na Shirika la Mwezi Mwekundu Nungwi Wilaya ya Kaskazini A
Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu
UAE Khalifa Abdurrahman Almarzooqi akizungumza katika hafla ya Uwekaji
wa Jiwe la Msingi Nyumba za Waathirika wa Maafa ya Upepo Mkali na Mvua
za masika zinazofadhiliwa na Shirika la Mwezi Mwekundu Nungwi Wilaya ya
Kaskazini A Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya
Zanzibar
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais Mihayo Juma Nhunga akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni
Rasmi katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Nyumba za Waathirika wa
Maafa ya Upepo Mkali na Mvua za masika zinazofadhiliwa na Shirika la
Mwezi Mwekundu Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Unguja.Ikiwa ni Shamra
shamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Hussein Ali Mwinyi
akitoa hotuba katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Nyumba za
Waathirika wa Maafa ya Upepo Mkali na Mvua za masika zinazofadhiliwa na
Shirika la Mwezi Mwekundu Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Unguja.Ikiwa ni
Shamra shamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/ MAELEZO ZANZIBAR.
……………..
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Hussein Ali Mwinyi amesema kukamilika kwa ujenzi wa nyumba za
waathirika wa upepo mkali na
mvua za masika kutaweza kutoa fursa kwa
wananchi walioathirika na mvua kubwa kuridhia na kufurahia makaazi hayo
kwa kaisi kikubwa.
Akiweka jiwe
la msingi katika kijiji cha waathirika wa maafa ya mvua huko Nungwi
Wilaya ya Kaskazini A amesema hatua hiyo itaweza kuwasaidia wananchi hao
kuwa katika makaazi salama na kuweza kuishi kwa amani
Alisema hatua
hiyo pia itaweza kuwapunguzia gharama katika kutafuta huduma za kijamii
ikiwemo elimu, maji, soko msikiti na huduma nyengine ambazo
zitawanufaisha na wananchi wengine tofauti.
Aidha alisema
Serikali ya awamu ya saba ilitoa kipaumbele kwa kuanzishwa kamisheni
ya maafa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wake juu ya athari
zinazowakumba kutokana na maafa hivyo ni vyema wananchi kutojenga sehemu
hatarishi mabondeni pamoja na njia kuu za maji ili kuepusha matatizo
yatayoweza kuwapata.
“Ni vigumu
kuzuiya majanga yasitokee hasa majanga ya kimaumbile kama vile kimbunga,
sunami, mafuriko,na mengineyo lakini ni rahisi kuyasuiya maafa
yasitokee maafa ambayo yanatokana na binaadamu kwa kujiepusha kujenga
sehemu hatarishi. “alisema Waziri wa Ulinzi
Waziri huyo
aliishukuru Shirika la Mwezi Mwekundu ya falme za Kiarabu UAE kwa
msaada huwo wa kuonyesha hali ya upendo na mshikamano mkubwa kwa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa juhudi waliyoiyonyesha kuweza
kufadhili mradi ambao utaweza kuokoa maisha ya walio wengi.
Hata hivyo
Waziri Husein Amewataka wakandarasi kumaliza ujenzi huo kwa wakati
uliopangwa ili wahanga wa maafa waweze kufaidika na huduma hiyo kabla
ya kufika Uchaguzi Mkuu ambao unatarajiwa mwishoni mwa mwaka huu.
Kwa upande
wake Balozi wa Nchi za falme za kiarabu Mhe, Khalifa abdulrahman
Almarzouk amesema jumuiya hiyo itaendelea kutoa misaada mbalimbali ya
kijamii kutokana na mahusiano yaliyopo baina ya nchi mbili hizo .
Ameahidi
kusaidia miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ya miundombinu ya maji,
elimu na afya kwa lengo la kuimarisha maisha ya wananchi wa Zanzibar.
Kwa Upande
wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Shaaban Seif Mohamed
amesema ujenzi wa kijiji hicho unatokana na athari za upepo mkali na
mvua kubwa za masika zilizotokea mwezi April na mei mwaka 2017 ambapo
nyumba zipatazo 6,005 ziliathirika kwa Unguja na Pemba.
Alifahamisha
kuwa nyumba nyingi zilizoathirika ni zile zilizomo katika maeneo
hatarishi yakiwemo mabondeni na njia asilia za maji hali hiyo ilipelekea
wana Shirika la Mwezi Mwekundu wa falme za kiarabu kutoa msaada kwa
kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema
ujenzi wa kijiji hicho umegawika katika awamu mbili tofauti ambapo awamu
ya kwanza ni kujenga nyumba I5 za familia thelathini kwa Nungwi Unguja
na Tumbe Pemba kwa muda wa mwaka, ujenzi huo unajengwa na Kampuni
Samkay Consultant , nyumba ambazo zinavyumba vitatu ukumbi, jiko, choo,
na stoo .
Kwa upande wa
Wahanga hao waliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na
Mashirika ya Kimaendeleo kwa kuweza kuwaunga mkono katika kipindi
ambacho kwao ni kigumu .
Aidha
wameomba kuendelea kutoa misaada na mashirikiano kwa jamii katika
miradi ya ujenzi wa nyumba hizo ili ziweze kuwasaidia wananchi wanaopata
matatizo .
Mmoja na
awamu ya pili ni kujenga huduma zilizobaki kwa muda wa miezi kumi ambapo
ujenzi huo umegharimu jumla ya shilling bilioni 1,614,299,188 sawa na
asilimia sitini.
No comments :
Post a Comment