***********************************
Happy Lazaro,Arusha.
Kutokana na mvua zinazoendelea
kunyesha katika mikoa mbalimbali nchini zimeendelea kuleta madhara
ikiwemo ya kambi za watalii wanaolala katika eneo la Mto wa mbu
wilayani Monduli kutokana na eneo hilo kufurika maji na hivyo kuleta
hofu kubwa miongoni mwa
wananchi hao.
wananchi hao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
Wakazi wa mji Mdogo wa Mto wa Mbu wilayani Monduli mkoani Arusha eneo la
Migungani A wameiomba serikali kunusuru maisha yao na hatari ya
kusombwa na mafuriko kutokana na kukosekana miundombinu imara
inayoruhusu maji ya mvua kutiririka ambayo yamekuwa yakikosa muelekeo
hivyo kutuama katika makazi,shule na kusababisha hofu kubwa kwa maisha
yao na hata kambi za watalii wanaolala eneo hilo kufurika maji.
Tangu mvua zimeanza kunyesha
katika msimu huu wakazi hao wamekuwa wakikumbana na adha kubwa ya maji
kujaa katika nyumba zao,mashamba,shule ambapo hali imezidi kuwa mbaya
zaidi pale baadhi ya kambi za watalii nazo kuonekana kujaa maji ,hivyo
kusababisha wageni kushindwa kulala katika eneo hilo.
Mmoja wa wakazi hao ,Catherine
Kubena, Dotto Mahimbo na mhandisi Kubene Joseph walisema hali
imeendelea kuwa mbaya kila kukicha huku wakihofia mvua zinazoendelea
kunyesha huenda zikaleta madhara Zaidi.
“Yaani sasa hivi mvua ikinyesha
watu hatuelewi tutoke nje au tubaki ndani maana maji yanajaa vitu
vinaharibika hata hatulali usingizi kweli maisha yetu yapo hatarini
tunaomba serikali iingilie kati suala hili kwa kutuongezea makalavati
ili tuweze kuishi kwa Amani”wananchi.
Aidha wananchi hao,walisema kuwa
kukosekana kwa makalavati ya kutosha na mifereji ambayo inaonekana
myembamba ikishindwa kuhimili kiwango cha maji yanayotiririka lakini pia
baadhi ikiwa imeziba ndio haswa chanzo cha tatizo lote
hili,ambapo wananchi hawa wanaamua kupaza sauti zao baada ya hali
kuendelea kuwa mbaya.
Hata hivyo ,Sekta ya utalii nayo
imeonekana kuathirika Zaidi ambapo Baadhi ya maeneo yaliyoathirika Zaidi
ni kambi ya kulala wageni ambazo zimejaa maji hivyo kusababisha wageni
kushindwa kulala katika kambi hizo.
“mifereji imeziba,mingine haina
uwezo wa kupitisha maji hivi unavyoona hali ni mbaya sana harufu ya maji
yamejaa kila mahali na tunahofia afya zetu huenda wakati wowote
pakatokea mlipuko wa magonjwa ya tumbo maana mashimo ya vyoo
yanazibuliwa kipindi hiki cha mvua.”alisema Janeth
Hata hivyo wakati wakisubiri
msaada wa serikali wananchi hao wameamua kujiongeza kwa kujitolea kwa
nguvu zao kuanza kuzibua mitaro ya maji lakini bado wanakabiliwa
na changamoto ya vitendea kazi duni.
No comments :
Post a Comment