Katibu tawala wa mkoa wa Arusha,Richard Kwitega akifafanua jambo.
………………………………………………………………………………………………………..
Happy Lazaro,Arusha.
Walimu wa shule binafsi nchini
wamelalamikia kutokushirikishwa katika usimamizi wa mitihani ya kitaifa
pamoja na usahihishaji licha ya kuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya
elimu nchini na kuchangia katika kukuza ubora wa elimu.
Akizungumza katika Mkutano wa
Chama cha Walimu wa Shule binafsi nchini ,Katibu Mkuu wa Chama hicho
Julius Mabula katika mkutano uliofanyika jijini Arusha ameiomba
serikali iwashirikishe katika kusimamia na kusahihisha mitihani ya
kitaifa kwani kwa miaka mingi wamekuwa hawashirikishi licha ya kuwa na
sifa stahiki kama walimu wa shule za serikali.
“sisi tunasifa kama vile
walimu wengine wa shule za serikali wanazo lakini kinachotushangaza
atushirikishwi katika swala lolote la usahihishaji mitiani wala
usimamizi wa hii mitiani kwa ufupi naweza sema tumetegwa sisi walimu
wa shule binafsi “Julius Mabula
Amesema kuwa watafurahi sana
kuona kwamba serikali inatambua uwepo wa kwa kuwashirikisha katika mambo
mbalimbali ya uhusuyo elimu kwani nguzo muhimu katika maendeleo ya
ellimu ni kushirikiana na kuchangia kukuza ubora wa elimu
Kwa upande wake mgeni
rasmi,Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema kuwa,
serikali imepokea maombi ya walimu wa shule binafsi katika kusimamia
mitihani ya kitaifa na watayafikisha kwenye ngazi husika ili yaweze
kufanyiwa kazi
“tumesikia maombi yenu na
tumeyapokea na napenda kuwahaidi kuwa tutafikiksha maombi haya katika
ngazi husika ili yaweze kufanyiwa kazi hivyo niwaambie usiwe na hofu
kwani serikali yenu ni sikivu na itafanyia kazi haya “amebainisha
Kwitega.
No comments :
Post a Comment