Monday, January 13, 2020

Wageni kutoka Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Kaskazini KCMC na Minneapolis Heart Institute Foundation ya nchini Marekani watembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa



Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na upandikizaji wa viungo kutoka Minneapolis Heart Institute Foundation ya nchini Marekani Vibhu Kshettry  akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha ubora wa huduma za matibabu ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Dkt. Tulizo Shemu  akimwelezea kuhusu upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua jinsi unavyofanyika kwa kutumia mtambo wa Cathlab walipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Kaskazini KCMC Dr. Gileard  Masenga ambaye aliambatana na wageni hao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi  akizungumza na wageni kutoka Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Kaskazini  KCMC na Minneapolis Heart Institute Foundation ya nchini Marekani walipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. Minneapolis Heart Institute Foundation ni wadau wakubwa wa Hospitali ya KCMC na hivi sasa wako katika mpango wa kutoka mafunzo kwa wataalamu wa afya pamoja na vifaa tiba kwa ajili ya uanzishwaji wa kitengo cha moyo katika Hospitali hiyo.
Dkt. John Reiling wa Minneapolis Heart Institute Foundation ya nchini Marekani akiangalia moja ya mashine zilizopo katika chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. Kulia  ni daktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa JKCI Godwin Sharau.
Wageni kutoka Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Kaskazini  KCMC na Minneapolis Heart Institute Foundation ya nchini Marekani wakiwa katika picha pamoja wakati wa ziara yao ya kutembelea  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Picha na JKCI

No comments :

Post a Comment