Mkemia Mkuu Dkt. Fidelice
Mafumiko akizungumza na wanahanari (hawapo pichani) wakati wa ziara ya
kampeni ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano
inayojulikana kama ‘Tunaboresha Sekta ya Afya’ mapema leo Jijini Dar es
salaam.
Mkurugenzi anayesimamia Idara ya Huduma ya usimamizi wa vinasaba, David Eliasi akizungumza katika tukio hilo.
Viongozi mbalimbali wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakiwa katika mkutano huo
***************************************
NA WAMJW,DSM
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia
Mkuu wa Serikali [GCLA] ipo katika mkakati wa kuanzisha Kanzi Data ya
taifa ya Vinasaba vya Binadamu [DNA] ambayo itakuwa ikitambua asili
ya kila Mtanzania na kuweza kusaidia chunguzi mbalimbali ikiwemo
majanga na kupata majibu kwa kina.
Hayo yameelezwa na Mkemia Mkuu
wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko wakati wa ziara ya kampeni ya
kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano inayojulikana kama
‘Tunaboresha Sekta ya Afya’ ambapo amesema kuwa;
Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha wanafikia malengo ya kusaidia jamii katika upande huo wa vinasaba.
“Kwa sasa tupo katika mpango wa
kuanzisha Kanzi Data ya Taifa ya Vinasaba ambapo eneo hilo kwa sasa
tutaliwekea kipaumbele katika bajeti ya fedha ya mwaka huu na tayari
tumeshaanza kutengeneza mpango kazi wazo dhana ya utengenezaji wake na
itajumlisha wadau mbalimbali na Serikali kupitia Wizara ya Afya na
wadau wengine”. Alisema Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Mafumiko.
Dkt. Mafumiko amebainisha kuwa,
kutokana na mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano kwa kuboresha
rasilimali watu, miundombinu ya utendeajji kazi na vifaa vya kisasa ndio
maana wamepewa jukumu hilo la kuanzishwa kwa Kanzi data hiyo sambamba
na kujumuisha wadau mbalimbali.
Nae Mkurugenzi anayesimamia
Idara ya Huduma ya usimamizi wa vinasaba, David Eliasi akizungumzia
suala hilo la Kanzi data, amesema kuwa, Mkemia wa Serikali ndio atakuwa
msimamizi na inajengwa na watanznia wenyewe huku akiwataka watanzania
wajivunie juu ya hilo.
“Serikali ya awamu ya Tano
imeweza kuongeza chachu na sasa tunajenga kanzi data ya Kitaifa ya
Vinasaba na inajengwa na Watanzania wenyewe.
Ni kitu cha kujivunia na timu ya
Kitaifa inasimamia huu ujenzi wakiwemo Wizara ya Afya ambayo ni mlezi
wetu, pia wapo EGav- Serikali mtandao, NIDA, RITA, NEC na taasisi
nyingi tu na wote hao wamekaa pamoja na wamekuja na dhana ya uanzishwaji
wa Kanzi data hii ya Kitaifa” alisema David Eliasi.
Ameongeza kuwa kuanzishwa kwa
kanzi data hiyo, itarahisisha upatikanaji wa haraka wa majibu ya
vinasaba kwani tayari sampuli zitakuwa zinapatikana kwenye data.
“Tutachukua muda mfupi na wa
haraka zaidi. Mfano lile janga la Morogoro la moto, ndugu wa marehemu
wangepatikana kupitia kanzi data hii na tungelipata majibu kwa haraka
na kwa wingi zaidi” alisema Davidi Eliasi.
Aidha, Mamlaka ya Maabara ya
Mkemia Mkuu wa Serikali imenunua mitambo tisa kwa gharama ya shilingi
bilioni 9.5 kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kemikali, sumu, madawa ya
kulevya na viambata.
Ambapo pia imeweza kusajili wadau 2426 mwaka 2019 kutoka wadau 4340 mwaka 2015/2016.
Mpaka sasa Mamlaka hiyo ya
Mkemia Mkuu imeendelea kuboresha huduma zake ikiwemo katika Kanda ya
Ziwa, Kaskazini, Nyanda za Juu Kusini na maeneo mengine ya Kanda.
No comments :
Post a Comment