Thursday, January 16, 2020

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) waongezewa ujuzi wa jinsi ya kutoa huduma ya dharula kwa mtu aliyepata tatizo la ghafla la kiafya na wataalamu kutoka Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani



Prof. Aubyn Marath ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani akiwafundisha baadhi ya wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi ya kutoa huduma ya dharula kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo. Wataalamu wa Shirika hilo wako JKCI kwa ajili ya kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto na watu wazima.
Baadhi ya wataalamu  wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Prof. Aubyn Marath ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji wa moyo (hayupo pichani) wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani wakati akiwafundisha jinsi ya kutoa huduma ya dharula kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo. Wataalamu wa Shirika hilo wako JKCI kwa ajili ya kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto na watu wazima
Daktari bingwa wa huduma ya  dharula wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani Richard Harper akiwafundisha baadhi ya wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi ya kutoa huduma ya dharula kwa mtoto  aliyepata tatizo la ghafla la kiafya. Wataalamu wa Shirika hilo wako JKCI kwa ajili ya kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto na watu wazima.
Mtaalamu wa utoaji wa huduma ya dharula wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani Mike Pyorala akiwafundisha baadhi ya wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi ya kutoa huduma ya dharula kwa mtu aliyepata tatizo la ghafla la kiafya. Wataalamu wa
Shirika hilo wako JKCI kwa ajili ya kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto na watu wazima
Picha na JKCI

No comments :

Post a Comment