| Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwajelwa, akizungumza na na Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida katika ziara yake ya kikazi mkoani humo jana. |
Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida wakimsikiliza Dkt. Mwanjelwa.
……………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Singida
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwajelwa amesema
Serikali baada ya kugundua kuwepo kwa uozo kwa
watumishi mbalimbali wanaokaimishwa nafasi mbalimbali waliamua kuja na waraka unaoelekeza kikomo cha mtumishi kukaimu katika nafasi husika.
watumishi mbalimbali wanaokaimishwa nafasi mbalimbali waliamua kuja na waraka unaoelekeza kikomo cha mtumishi kukaimu katika nafasi husika.
Mwanjelwa
aliyasema hayo jana wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Singida katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.
“Suala
la kukaimu kwa muda mrefu ndiko kuna sababisha kuwepo na uozo mkubwa
katika sehemu zetu za kazi kutokana na watendaji hao kutokuwajibika kwa
ufanisi” alisema Mwanjelwa.
Naibu
waziri huyo amewataka watumishi wote wa halmashauri hususani mkurugenzi
na wakuu wa idara kufanya kazi kwa ushirikiano ikiwa ni pamoja na
kupokea ushauri wa kitaalamu unao tolewa na akasisitiza sauala la
mafunzo katika kazi ili kuwaongezea ujuzi watumishi hao.
Katika ziara hiyo mbali na
kukutana na kutatau kero mbalimbali za watumishi katika halmashauri za
mkoa wa Singida pia anapitia kuangalia utekelezaji wa mpago wa kunusuru
kaya Masikini TASAFKatika ziara hiyo mbali na kukutana
na kutatau kero mbalimbali za watumishi katika halmashauri za mkoa wa
Singida pia anapitia kuangalia utekelezaji wa mpago wa kunusuru kaya
Masikini TASAF
No comments :
Post a Comment