Waziri Wa ujenzi ,uchukuzi na
Mawasiliano muhandisi Isack Kamwene akimuelekeza mkandarasi eneo LA
uwanja lililopo jiji Arusha kwa ajili ya ujenzi Wa jengo LA makao makuu
ya mashirika ya posta Kwa nchi za Afrika ,litakalo gharimu kiasi cha
shilingi za kitanzania Bilioni 33
Waziri Wa ujenzi ,uchukuzi na
Mawasiliano muhandisi Isack Kamwene akimuonyesha mkandarasi ramani ya
jengo hilo LA makao makuu ya mashirika ya posta Afrika ,jengo hilo
linatarajiwa kuwa na gorofa 16 na linatarajiwa kukamilika ndani ya
mienzi 30
Mkandarasi Wa kampuni ya Beijing
Construction Enginering Group ,Liang Li akimueleza Waziri kuwa
watakamilisha ujenzi huo Wa jengo LA makao makuu ya mashirika ya posta
Afrika kwa wakati (picha na Woinde Shizza,Arusha).
……………..
Na Woinde Shizza ,Arusha
Waziri Wa ujenzi
,uchukuzi na mawasiliano muhandisi Isack Kamwele Leo amemkabithi
rasmi kiwanja kwa ajili ya ujenzi Wa jengo la makao makuu ya mashirika
ya Posta Afrika mkandarasi Wa kampuni ya Beijing construction
,Liang Li jengo litakalo jengwa ndani ya jiji LA Arusha na
litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 30 .
Akizungumza wakati
Wa kukabidhi eneo hilo alisema kuwa ujenzi huo umekuja muda muafaka
kwa kipindi cha RaisWa awamu ya Tano kiongozi ambaye anafata nyayo za
baba Wa Taifa mwalimu Julius Nyerere na anaamini kuwa ujenzi huo
utakamilika kwa wakati
“Kuna nchi 45
wanachama Wa mashirika ya posta katika nchi za Afrika 1980 walikaa na
kukubaliana makao makuu ya mashirika ya posta yawe hapa Tanzania na
baba Wa Taifa akakubaliana nao na wakapangwa yajengwe Arusha na ndio
maana katika kuathimisha miaka 40 ya mashirika haya tumeamua tuanze
kujenga jengo la makao makuu ya mashirika haya ya posta Afrika” alisema
Kamwele
Alisema jengo hilo
litakuwa na gorofa 16 na adi kumalizika litagharimu kiasi cha shilingi
milioni 17 za kitanzania na linatakiwa kujengwa na kumalizika kwa
kipindi cha miezi 30 huku akimtaka mkandarasi Wa jengo hilo kujenga
katika ubora unao takiwa na viwango vya serikali .
Aliwataka wakandarasi
hawa kuhakikisha wafanyakazi wao ambao wanatoka nje ya nchi kuja na
nyaraka zote za uhamiaji pamoja na vibali vya kufanyia Kazi hapa
nchini.
“Jengo hilo ni makao
makuu ya mashirika ya posta Afrika hairuhusiwi mtu yeyote asie husika
kuingia katika eneo hili bila kibali kutoka kwa wahusika ,eneo hili ni
LA kimataifa haitakiwi kuingia bila kibali iwapo MTU atakutwa hatua
Kali za kisheria zitachukuliwa juu yake” alibainisha
Kwa upande wake
mkurugenzi Mkuu Wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania Dk Jones Kilembe
alitumia muda huo kushukuru serikali kwa jinsi ilivyoonyesha usimamizi
na ufuatiliaji hadi kufikia hapa tulipofika katika ujenzi wa jengo hilo
la makao makuu ya mashirika ya posta Tanzania.
Aliwataka wananchi Wa
Arusha kutoa ushirikiano katika maswala ya ulinzi hats ikitokea katika
eneo la uchangiaji ,aliongeza kuwa watamsimamia vyema mkandarasi huyu na
kuhakikisha anamaliza Kazi kwa muda uliopagwa na ikiwezekana hata kabla
ya muda uliopangwa kufika
Naye Mkuu mkoa Wa
Arusha Mrisho Gambo ameshukuru Wizara ya uchukuzi,ujenzi na mawasiliano
pamoja na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kujenga makao makuu
ya mashirika ya posts nchi za Afika jijini hapa ambapo alisema kwa
nafasi yake atashirikana nao vyema katika kutatua vikwazo vyote
vilivyopo ndani ya uwezo wake katika nafasi ya ngazi ya mkoa ili
kuhakikisha mkandarasi anamaliza Kazi kwa wakati.
No comments :
Post a Comment