Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
ya Benjamin Mkapa(BMH) Dk.Alphonce Chandika, akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu wagonjwa waliopandikizwa figo katika
hospitali hiyo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya
figo kutoka Japan, Prof.Kobayashi Shuzo,akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu wagonjwa waliopandikizwa figo.
Mkuu wa chuo cha Tiba cha UDOM
Prof.Ipyana Mwampagatwa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu wagonjwa waliopandikizwa figo katika hospitali ya
Benjamin Mkapa.
Daktari bingwa wa magonjwa ya figo
katika Hospitali ya Benjamin Mkapa(BMH) Dk.Kessy Shija,akitoa ufafanuzi
kuhusu wagonjwa waliopandikizwa figo katika hospitali hiyo.
Mmoja wa wanufaika waliopandikizwa
figo Bi. Leah Nkonoki,akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani)
jinsi alivyoweza kuokoa maisha yake kwa kupandikizwa figo.
Mkurugenzi wa Hospitali ya
Benjamin Mkapa(BMH) Dk.Alphonce Chandika, akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu wagonjwa waliopandikizwa
figo.
PICHA ZOTE NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
………………………….
Na Alex Sonna,Dodoma
Hospitali ya Benjamin Mkapa(BMH),
imefanikiwa kufanya upandikizaji figo kwa wagonjwa wengine wanne na
hivyo kufikia 11 tangu kuanza kwa huduma hiyo.
Sambamba na hilo, upandikizaji huo umeweza kuokoa mamilioni ya fedha ambayo
yangetumika kutibu wagonjwa nje ya nchi.
Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi
wa Hospitali hiyo, Dk.Alphonce Chandika, alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu wagonjwa waliopandikizwa figo.
Amesema awali kulikuwa na wagonjwa
saba na Januari 6, mwaka huu wamewafanyia wagonjwa wanne ambao wote
wanaendelea vyema pamoja na waliowapatia figo.
Ameeleza kutolewa kwa huduma hiyo
kumeokoa fedha nyingi ambazo zilikuwa zikitumika kutibu wagonjwa hao nje
ya nchi ikiwemo nchini India.
Amefafanua upandikizaji figo kwa
mgonjwa mmoja kwenye hospitali hiyo unagharimu kati ya Sh.Milioni 22
hadi 25, na kwamba gharama ya matibabu hayo kwa nje ya nchi ni zaidi ya
Sh.Milioni 100.
Dk.Chandika amesema gharama
inayotumika kwa mgonjwa mmoja nje ya nchi inaweza kuhudumia wagonjwa
watano katika hospitali hiyo na kwamba kwa wagonjwa saba wa awali
ziliokolewa Sh.Milioni 700.
“Kwa wagonjwa ambao tumewafanyia huduma hii hakuna mgonjwa hata mmoja aliyepoteza maisha, wote wanaendelea vizuri,”amesema.
Aidha, amesema upandikizaji huo
ulikuwa ukifanyika kwa kushirikiana na Chuo Kikuu ch Dodoma(UDOM) pamoja
na wataalam kutoka Tokushukay Medical Corporation nchini Japan ambao
baada ya upandikizaji huo wa watu wanne itakuwa ni mwisho kuja jopo
kubwa kutokana na madaktari wa kitanzania kukomaa kwenye utoaji huduma
hiyo.
Dk.Chandika amesema hospitali hiyo
na wataalam wake wapo tayari kutoa huduma bora ya upandikizaji kutokana
na ujuzi walioupata kutoka Japan.
“Tuna madaktari wanne ambao
wamepata mafunzo kuhusu upandikizaji figo, hawa wameenda Japan mara
mbili sio kwenda kuangalia bali kushiriki kabisa kwenye upasuaji na
upandikizaji maana kule wenzetu wanafanya mara kwa mara,”amesema
Ameeleza kuwa wataalam hao wataitwa au kuombwa ushauri kama itatokea mmoja wa wagonjwa ana shida ambayo si ya kawaida.
Naye, Mwenyekiti wa jopo la
wataalam kutoka Japan, Prof.Kobayashi Shuzo, amepongeza Tanzania kwa
kuimarisha huduma za kibingwa ikiwemo za upandikizaji figo na kwamba
hospitali hiyo mbali na kutoa huduma kwa watanzania wataweza kuhudumia
pia wanaotoka mataifa mengine.
Kwa upande wake, Mmoja wa
wanufaika wa huduma hiyo, Leah Nkonoki, amesema tangu amepandikizwa figo
mwaka 2018 hajawahi kuumwa ugonjwa wowote na anaendelea na shughuli
zake na alipewa figo na dada yake.
No comments :
Post a Comment