Baadhi ya vitabu ambavyo vitasambazwa katika halmashauri hapa nchini kwaajili ya kutumika kufundishia mashuleni.
Mkurugezi Mkuu wa TET Dkt.Aneth Komba akiongea katika hafla ya uzinduzi wa usambazi wa vitabu kwenda kwenye halmashauri nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akizindua wa usambazaji
wa vitabu kwenye halmashauri hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa usambazaji wa vitabu kwenda kwenye halmashauri hapa
nchini.
********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Taasisi ya Elimu
Tanzania TET imetumia Bilioni 12na milioni 600 kuzalisha vitabu vya
shule za awali,msingi na sekondari kwa kutumia mapato ya ndani ikiwa ni
muendelezo wa
maboresho ya sera ya elimu bila malipo ilianzishwa na
serikali ya awamu ya tano chini ya jemedari Rais Dk.John Maguifuli.
Akizungumza
kwenye hafla ya uzinduzi wa usambazaji wa vitabu hivyo kwenda kwenye
halmashauri, Mkurugezi Mkuu wa TET Dk.Aneth Komba alisema fedha
zilizotumika kuzalisha vitabu hivyo ni jitihada za Rais katika
kupandisha hadhi ya sera ya elimu bila malipo kwa kutumia mapato ya
ndani.
Dkt.Aneth alisema
jumla ya nakala z vitabu vyote vilivyozalishwa ni 2,962,155 na
viongozi ni 224.000 i vya elimu ya sekondari ni 690,000,elimu ya awali
ni vitabu 719,905,elimu ya msingi ni vitabu 500,000 pamoja na vitabu
vya muongozo vya walimu ni 400,000.
Alisema vitabu
hivi vikawe ni chachu ya maendeleo katika shule za awali mpaka sekondari
ili vikasaidie kutatua changamoto za vitabu walizokuwa nazo katika
shule.
Alifafanua kuwa
vitabu hivi vitasambazwa katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara kwa
kupitia kwenye halmashauri za mikoa yote husika.
“Naziomba
halmashauri zisiviache vitabu kwenye ofisi vikaliwa na panya wanatakiwa
kuvisambaza kwenye shule zote kuanzia shule za awali mpaka za sekondari
na wahakikishe ni kweli vitabu hivyo vinawafikia wahusika na kutumiwa
na wanafunzi waliokusudiwa”. Alisema Dkt.Aneth
Kwa mujibu wa
Mkurugezi Mkuu alisema sekta ya elimu kwa sasa imeimarika kupitia mpango
wa elimu bila malipo unasonekana matokeo yake kupitia matokeo ya kidato
cha nne ya mwaka huu ambayo ndiyo matokeo ya mwanza ya mpango wa elimu
bila malipo ambayo yameongezeka kwa asilimia 80.7 wakati yale ya 2015
yalikuwa ni asilimia 67.
Vile vile alisema
kwa sasa shule za kata zinaongoza kufanya vizuri pamoja na wananchi
kuzibeza kuwa hazina ubora kupitia vitabu hivyo vikatatue changamoto na
kuboresha elimu ya watoto.
Kwa upande wa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard
Akwilapo alisema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John
Magufuli imeipa kipaumbele sekta ya elimu hivyo wananchi wanatakiwa
kumuunga mkono Rais katika jitihada zake za elimu bila malipo.
Dkt.Akwilapo
alisema serikali ya awamu ya tano imepokea Dola 90 kwa ajili ya uandishi
wa vitabu,kuongeza vifaa vya kufundishia,kutoa mafunzo kwa walimu na
kuboresha miundombinu ya shule.
Alisema sekta ya elimu ni sekta muhimu kwa jamii analishukuru jeshi la wananchi wa Tanzania kupitia Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo kwa kutoa mchango wao katika kufanikisha zoezi hili la usambazaji wa vitabu katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
No comments :
Post a Comment