Friday, January 17, 2020

MTAKWIMU KUTOKA OFISI YA MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI ATOA TAKWIMU ZA UINGIAJI WAGENI ZANZIBAR.



Mkurugenzi Masoko Kamisheni ya Utalii Dkt,Miraji Ukuti Ussi akizungumza kuhusiana na uingiaji wageni katika Mkutano  na Waandishi wa Habari kuzungumzia Takwimu za Uingiaji Wageni Nchini ambapo imeonekana kupanda kwa Mwezi wa Disemba 2019 kwa Wageni 60,685.sawa na Asilimia 14.9.Ikilinganishwa na wageni 52,828 walioingia mwezi wa Disemba 2018 hafla iliofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Mazizini Zanzibar. 
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Kitengo cha Utalii katika idara ya Takwimu za Kiuchumi Bakari Ali akitoa takwimu za  Uingiaji Wageni Nchini ambapo imeonekana kupanda kwa Mwezi wa Disemba 2019 kwa Wageni 60,685.sawa na Asilimia 14.9.Ikilinganishwa na wageni 52,828 walioingia mwezi wa Disemba 2018 hafla iliofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Mazizini Zanzibar. 
Mkuu wa Idara ya Takwimu za Kiuchumi katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Abdul Ramadhan akitolea ufafanuzi baadhi ya maswala yalioulizwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuzungumzia Takwimu za Uingiaji Wageni Nchini ambapo imeonekana kupanda kwa Mwezi wa Disemba 2019 kwa Wageni 60,685.sawa na Asilimia 14.9.Ikilinganishwa na wageni 52,828 walioingia mwezi wa Disemba 2018 hafla iliofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Mazizini Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
*****************************
Na Mwashungi Tahir     Maelezo     17-1-2020.
Imeelezwa  kwamba idadi ya wageni walioingia nchini kwa mwaka 2019 ni 5,38,264 ambapo ni
sawa na ongezeko la asilimia 3.4 ikilinganishwa na wageni   520,809 walioingia mwaka 2018.
Akiwasilisha takwimu za uingiaji wa wageni nchini wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari huko katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizizni,Mkuu wa kitengo cha Takwimu za Utalii katika Ofisi hiyo Abdul-malik Bakari Ali amesema jumla ya wageni 474,345 wameingia nchini kwa kupitia usafiri wa Anga na 63,919 wameingia kwa kupitia usafiri wa Bandarini.
Alisema Nchi  ya Itali inayoongoza kwa kuingiza idadi kubwa ya  wageni na kuchangia asilimia 11.4 kwa mwaka 2019,ikifuatiwa na Marekani  iliofikia asilimia 8.1 ambapo Ujerumani iliochangia asilimia 7.9.
Aidha alisema kwa mwezi wa Disemba 2019 idadi ya wageni walioingia nchini ni 60,685 sawa na ongezeko la asilimia 14.9 ikilinganishwa na wageni 52,828 walioingia mwezi wa Disemba mwaka 2018.
Kwa upande wake Mkurugenzi Masoko kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dkt. Miraji Ukuti Ussi  alisema kuimarika kwa miongombinu,kuwepo kwa Hoteli zenye ubora wa kuvutia Watalii imesababisha kuongezeka kwa Idadi ya Watalii nchini.
Mbali na hayo Dkt.Ukuti alisema miongoni mwa vivutio hivyo ni pamoja na Magofu ya Bihole Bungi na Hoteli ya Verde yenye hadhi ya nyota 5,hali ambayo imechangia kuongezeka kwa pato la Serikali.

No comments :

Post a Comment