…………………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya ndani
ya Nchi, Kangi Lugola leo amefika Makao Makuu ya Ofisi za Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhojiwa. Kangi amewasili
Katika Ofisi jizo zilizopo eneo la Jamhuri jijini Dodoma majira 7:24
asubuhi kwa
ajili ya kuhojiwa ambapo anatarajiwa kutoka 9:30asubuhi.
Kangi ambaye kwa sasa ni Mbunge wa
Mwibara (CCM) wenzake watatu ambao ni aliyekuwa Kamishna Jeneral wa
Zimamoto na uokoaji, Thobias Andengenye, Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jacob Kingu na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,
Mhandisi Hamad Yusuph Masauni wote watahojiwa leo kwa nyakati tofauti.
Wote wanne wanahojiwa kufuatia
agizo la Rais, Dk.John Magufuli kufuatia mkataba ilioingiwa na wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi wa Sh.trilioni 1. “Watu wamekosa uadilifu, hivi
karibuni kulikuwa na mkataba mmoja wa ajabu unaotengenezwa Wizara ya
Mambo ya Ndani wenye thamani ya zaidi ya Sh1 trilioni.
Mradi huo umesainiwa na kamishna
jenerali wa Zimamoto,”alinukuliwa rais Dk.Magufuli katika sehemu ya
hotuba yake. Thobias Andengenye, ataingia kuhojiwa majira ya 9:30
asubuhi, Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Jacob Kingu ataingia kuhojiwa majira ya 2:00, mchana na Naibu Waziri wa
Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni ataingia kuhojiwa majira ya
saa 6.00 jioni.
No comments :
Post a Comment