Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina
Chonjo akifunga kikao cha wadau walioshiriki kuandaa taarifa ya Nchi ya
Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa kutokomeza vitendo vya ubaguzi
dhidi ya wanawake uliofanyika mjini morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo
ya Jinsia Bibi Mboni Mgaza akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro
Regina Chonjo aliyekuwa Mgeni rasmi wakati wa kufunga mkutano wa wadau
walioshiriki kuboresha taarifa ya Nchi ya utekelezaji wa Mkataba wa
Kimataifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake uliohitimishwa leo
mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Shirika la LANDESA
Dkt. Monica Muhoja (kulia) akipongeza uongozi wa Wizara ya Afya,
Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuwashirikisha wadau
katika mchakato wa kuandaa Taarifa ya Nchi ya Utekelezaji wa Mkataba wa
Kimataifa wa Kutokomeza vitendo vya ubaguzi dhidi ya wanawake kwa
kipindi cha mwaka 2015- 2019 katika kikao kazi ilichohitimishwa leo
mjini Morogoro.
Baadhi ya wadau walioshiriki
kikao akzi cha kuboresha Taarifa ya Nchi ya utekelezaji wa Mkataba wa
kimataifa wa Kutokomeza vitendo vya ubaguzi dhidi ya wanawake
wakifuatilia kwa makini nasaha za Mgeni Rasimi Mhe. Regina Chonjo.
…………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu Morogoro
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi.
Regina Chonjo amewataka wadau wa haki na utetezi wa wanawake kuendeleza
juhudi za Serikali ili kuhakikisha wanawake wanalindwa dhidi ya
ubaguzi
wa aina yoyote na kushiriki katika fursa za maendeleo na ustawi wao.
Bi. Chonjo alisema hayo wakati wa
kuahirisha Kikao cha wadau wa Kitaifa waliokutana mjini Morogoro kwa
lengo la kuboresha Taarifa ya Nchi ya Utekelezaji wa Mkataba wa
Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW).
Aidha Bi. Chonjo aliwapongeza
wadau kwa kuweza kuainisha mafanikio yaliyofikiwa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuzuia ubaguzi dhidi ya wanawake
na wasichana kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi 2019 akilitaja jambo hilo
kuwa limetokana na utendaji wa pamoja.
’’Kazi hii ya kuandaa Taarifa
ya Nchi ambayo mumeifanya kwa muda wa siku tatu itaboresha shughuli
zilizofanyika na kuonesha jinsi Tanzania ilivyotekeleza masuala ya
kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake na pia kuwawezesha kiuchumi,
kisiasa na kijamii’’. Aliongeza Bi. Chonjo.
Aidha Bi. Chonjo pia alisema
idadi ya wanawake nchini Tanzania ni kubwa ukilinganisha na idadi ya
wanaume uku akitaja takwimu zinaonesha kuwa kuna takriban asilimia 51 ya
wanawake ukilinganisha na wanaume na kati ya hao 80% wanaishi vijijini
wakijiajiri katika shughuli za kilimo, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa
kuwalinda wanawake dhidi ya ubaguzi na aina zote za ukatili wa kijinsia
ili kushiriki nafasi za maendeleo.
’’Tukitambua kuwa idadi ya
Wanawake nchini ni kubwa kwa asilimia 51 ukilinganisha na idadi ya
wanaume hoja hii inakuwa msingi wa kuwekeza katika kukuza ushiriki wa
wanawake ambapo takriban asilimia 80 ya wanawake hao wanaishi vijijini
wakiwa wamejiajiri katika sekta ya kilimo, hivyo kuna uhitaji mkubwa wa
kupinga ubaguzi dhidi ya wanawake’’.Alisisitiza kiongozi huyo wa Wilaya.
Aidha Bi. Chonjo alizitaja juhudi
za serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake
nni pamoja na kuanzisha Madawati ya Jinsia na Watoto 420 katika Vituo
vya Polisi kwa lengo la kuwezesha kupata haki na huduma stahiki kwa
wanawake na kuongeza kuwa madawati haya yameongeza ari ya wananchi
kujiamini na kuvunja ukimya katika utoaji taarifa za vitendo vya ukatili
kwenye maeneo ya jamii.
Aidha Bi. Chonjo alivitaja
Vituo vya pamoja vya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia
kuwa vimeanzishwa katika mikoa sita ya Tanzania Bara ambavyo ni Dar es
Salaam, Pwani, Mwanza, Mbeya, Iringa na Shinyanga vimewesha utoaji wa
huduma stahiki kwa waathirika akivitaja kuwa hatua muhimu iliyochokuliwa
na serikali kupambana na vitendo vya ukatili hapa Nchini.
Bi. Chonjo alitaja hatua nyingine
iliyochukuliwa na Searikali kupuna na vitendo vya ukatili kuwa ni
kufanya marekebisho ya Sheria ya Elimu na kulifanya kosa la kumpa mimba
au kuoa au kuolewa mwanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuwa kosa
la jinai na pale inapothibitika adhabu yake ni kifungo cha miaka 30
marekebisho haya yamesaidia kupunguza matukio ya mimba za utotoni.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa
Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bibi Mboni Mgaza ameeleza kuwa Taarifa hii
ya Tisa ya Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza aina zote
za ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW)itawasilishwa Umoja wa Mataifa Mwezi
Machi 2020 ikiwa imeunganisha taarifa ya Tanzania Bara na Tanzania
Zanzibar.
No comments :
Post a Comment