Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Philip Isdor
Mpango (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Global Fund Barani Afrika
Bw. Linden Morrison, walipokutana na kufanya mazungumzo Jijini Dodoma ambapo
pande hizo mbili zimeahidi kuendelea kushirikiana ambapo Global Fund imeahidi
kuipatia Tanzania dola milioni 600 mapema Januari mwaka 2021.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb), akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Global Fund- Afrika Bw. Linden Morrison
hayupo pichani wakati wa kikao kati ya Waziri wa Fedha na Mipango na uongozi wa
Global Fund kilichofanyika Jijini Dodoma. Kushoto ni Kaimu Kamishina wa Idara
ya Fedha za nje, Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Sauda Msemo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
Isdor Mpango (Mb), akiwa na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango
wakati wa kikao na uongozi wa Global Fund Afrika uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha na Mipango Bw. Adolf Ngunguru na Kulia ni Kaimu Kamishina Idara ya Fedha
za nje, Bi. Sauda Msemo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.
Adolf Ndunguru, akifuatilia jambo katika kikao kati ya Waziri wa Fedha na
Mipango na Uongozi wa Global Fund Afrika. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi
wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma. Kushoto ni Kaimu Kamishina wa Sera
-Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. William Mhoja.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Philip Isdor
Mpango (Mb), akisalimiana na Mkuu wa Global Fund Barani Afrika Bw. Linden
Morrison, walipokutana na kufanya mazungumzo Jijini Dodoma ambapo pande hizo
mbili zimeahidi kuendelea kushirikiana ambapo Global Fund imeahidi kuipatia
Tanzania dola milioni 600 mapema Januari mwaka 2021
Mtalaamu wa Fedha Mwandamizi kutoka Taasisi ya Global
Fund -Afrika Bi. Shevone Corbin akifafanua jambo katika kikao na Waziri wa
Fedha na Mipango uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini
Dodoma. Kulia kwake Mkuu wa Taasisi ya Global Fund -Afrika Bw. Linden
Morrison.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Philip Isdor
Mpango (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Global Fund
-Afrika na Viongozi na Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, baada ya kikao
kati ya Waziri wa Fedha na Taasisi ya Global Fun, Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)NA RAMADHANI KISIMBA, WFM-DODOMA
SERIKALI ya
Tanzania itanufaika na msaada wa dola za Marekani milioni 600 zitakazotolewa na
Taasisi ya Global Fund mwezi Januari mwakani kwa ajili ya kusaidia kukabiliana
na maradhi ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria katika kipindi cha miaka
mitatu.
Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mkuu wa Mfuko
huo Barani Afrika Bw. Linden Morrison, alipokutana na kufanya mazungumzo na
Waziri wa Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Amesema kuwa fedha hizo sawa na takriban shilingi za
Tanzania trilioni 1.4 zitatumika kuimarisha afya kwa kupambana na magonjwa ya
Ukimwi, Kikufua Kikuu na Malaria ambapo vifaa tiba na vitendanishi mbalimbali
vitanunuliwa kupitia msaada huo katika kipindi cha miaka mitatu (2021-2023).
Ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka 15 ambacho
taasisi yake imekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania, Mfuko wake tayari umetoa
msaada wa dola za Marekani bilioni 2 kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya hususan
katika mapambano dhidi ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,
ameishukuru Taasisi hiyo ya Kimataifa ya Global Fund kwa mchango mkubwa
iliyoipatia Tanzania katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo hasa malaria,
ugonjwa unaoongoza kusababisha vifo vya watanzania wengi.
Dkt. Mpango aliahidi kwamba fedha hizo zitatumika
kikamilifu na kama ilivyokusudiwa ili zilete matokeo chanya kwa kuwafikia
walengwa nchini kote.
‘‘Nimefurahi kwa sababu nina matumaini kuwa tumepata
nguvu ya kupambana na magonjwa haya makubwa, ili Watanzania wawe na afya njema
na waweze kujenga uchumi wa nchi yao’’ Alisema Mhe. Mpango.
Aidha Dkt. Mpango alisema katika kikao hicho
wamejadili namna ya kuboresha zaidi ushirikiano uliopo kati ya pande hizo mbili
ikiwemo kuangalia namna ya kutoa msamaha wa kodi kwenye vifaa yakiwemo magari
ya kubebea wagonjwa na dawa zinazoingizwa nchini na Taasisi hiyo kwa ajili ya
mradi huo.
“Aidha, Ili kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na
Taasisi ya Global Fund, nchi itahakikisha inakuwa na ushiriki mpana katika Bodi
ya Wakurugenzi ya Mfuko huo ili sauti ya nchi iweze kusikika zaidi” aliongeza
Dkt. Mpango
Kuhusu ubadhirifu wa zaidi ya dola za Marekani 400,000
zinazodaiwa kufujwa na baadhi ya Watendaji wa Serikali wanaotekeleza mradi huo
hapa nchini, Dkt. Mpango ameuahidi Mfuko huo kwamba Serikali itachunguza na
kuwachukulia hatua kali watu wote waliohusika na vitendo hivyo.
No comments :
Post a Comment