Mbunge
wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (mwenye suti
nyeupe) akitembelea na kukagua ujenzi wa zahanati ya Bushushu iliyopo
katika kata ya Lubaga katika Manispaa ya Shinyanga leo Januari 3,2020
wakati akiendelea na ziara yake Jimboni. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mbunge
wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (mwenye suti
nyeupe) akizungumza kwenye zahanati ya Bushushu na kuahidi kupeleka
moramu kwenye zahanati hiyo.
Mbunge
wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (mwenye suti
nyeupe) akipokea maelezo kuhusu ujenzi wa zahanati ya Bushushu ambayo
ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi na mbunge kuchangia mifuko ya
saruji na sasa ujenzi umefikia hatua ya renta.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akikagua jengo la zahanati ya Bushushu.
Muonekano wa jengo la zahanati ya Bushushu.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi na kata ya Lubaga wakati wa ziara yake leo Januari 3,2020.
Mbunge
wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza
na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi
na kata ya Lubaga wakati wa ziara yake leo Januari 3,2020.
Katibu
Msaidizi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rashid Mnunduma akizungumza
wakati wa kikao cha Mbunge Stephen Masele na Wajumbe wa kamati ya siasa
Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi na kata ya Lubaga.
Mwenyekiti
wa CCM kata ya Lubaga Anord Makombe akizungumza wakati wa kikao cha
Mbunge Stephen Masele na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi
CCM wa ngazi ya matawi na kata ya Lubaga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius
Masele akizungumza na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM
wa ngazi ya matawi na kata ya Kambarage wakati wa ziara yake leo
Januari 3,2020.
Diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata ya Kambarage.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM
wilaya ya Shinyanga Mjini Amri Migeyo wakati Mbunge wa Jimbo la
Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza na Wajumbe wa
kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi na kata ya
Kambarage wakati wa ziara yake leo Januari 3,2020.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga
Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza na Wajumbe wa kamati ya
siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi na kata ya Mjini wakati
wa ziara yake leo Januari 3,2020.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mhe.
Masele amefika katika zahanati ya Bushushu leo Ijumaa Januari 3,2020
ikiwa ni mwendelezo wa ziara katika Jimbo lake kukagua utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wajumbe wa kamati za
siasa CCM ngazi ya matawi na kata.
“Nimeridhishwa
na kasi ya ujenzi wa zahanati ya Bushushu yenye vyumba 15 ambayo mimi
mwenyewe niliuanzisha kwa kwa kuchangia mifuko 100 ya saruji.Niwapongeze
sana wananchi na wadau mbalimbali kwa ushirikiano wenu kushiriki ujenzi
wa zahanati hii.
“Nimerudi
tena kwa mara pili kuwaunga mkono wananchi ili tukamilishe ujenzi huu
na wananchi waanze kupata huduma za afya. Nitaleta moramu kujaza jengo
hili pamoja na kutafuta fedha lakini pia nitazungumza na Mkurugenzi wa
halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili amalizie ujenzi kwa kupaua
jengo hili kwani sisi wananchi tumeshajenga boma. Kwa utaratibu uliopo
wananchi wakijenga boma,serikali inatakiwa kumalizia ujenzi”,alieleza Masele.
Mbunge
huyo alisema serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo
ya barabara,maji na umeme huku akibainisha kuwa huwezi kuzungumzia
maendeleo ya mji wowote bila kugusa miradi hiyo ambayo inahitaji
mikakati mizuri kuitekeleza badala ya bla bla.
“Huwezi kutenganisha maendeleo ya Shinyanga Mjini na Mbunge wa Jimbo. Tunayo ‘Master Plan’ tuliyoitengeneza tangu mwaka 2011,Huu ni mkakati
wa kuboresha mji wa Shinyanga uwe wa Kisasa. Utekelezaji wa awamu ya
kwanza naweza kusema umeisha mwaka 2019 ambapo tumefanikiwa kujenga
barabara za lami kilomita 13 za kupitia Benki ya dunia. Na katika awamu
ya pili tunatarajia kujenga kilomita 18 za barabara za lami zingine
mpya.
Hizi
kilomita 13 za barabara tulizojenga hadi sasa tu zimeufanya mji wa
Shinyanga upendeze kiasi hiki ambapo kuna barabara za lami na taa zake.
Je tukiongeza barabara zingine kilomita 18 muonekano wa mji
utakuwaje?,ndiyo maana nikisema tunataka Shinyanga iwe mji wa Kisasa
kuna baadhi ya watu hawanielewi kwa sababu hawajui mipango iliyopo”,alifafanua Masele.
Masele
alisema mpango uliopo ni kuhakikisha kata zote za Jimbo la Shinyanga
Mjini zinaunganishwa kwa barabara za lami na kuwaomba wananchi kutumia
fursa ya mji wa Shinyanga kufanya shughuli za kujiinua kiuchumi.
Mbali
na kutembelea kata ya Lubaga, Mhe. Masele ambaye pia ni Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) akiwa ameambatana na Wajumbe wa
kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini
amekutana na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi
ya matawi na kata ya Mjini na Kambarage.
No comments :
Post a Comment