Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa
Sweeden Nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg wakati Balozi Sjoberg
alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar es salaam leo
Januari 17,2020. kushoto ni katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais )
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana
na Balozi wa Sweeden Nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg wakati Balozi
Sjoberg alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar es salaam
leo Januari 17,2020 kwa ajili ya kuzungumza na Makamu wa Rais.
***************************
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema
Tanzania itahakikisha inazidi kuimarisha Uhusiano wake na Sweeden katika
Sekta ya Elimu, Uwekezaji wa Biashara, Utalii na Mazingira.
Makamu wa Rais
ameyasema hayo leo Januari 17,2020 Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es
Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweeden
Nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg.
Aidha Makamu wa
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Balozi Sjoberg kwamba
Tanzania itaendeleza kukuza na kuimarisha Ushirikiano na Uhusiano kati
ya Nchi mbili hizi katika Sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Uwekezaji wa
kibiashara na Mazingira wakati Tanzania ikiwa mbioni kuelekea katika
Uchumi wa Viwanda.
Nae Balozi wa
Sweeden Nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg amemuahidi Makamu wa Rais
kwamba Nchi yake itashirikiana Bega kwa Bega na Tanzania katika
kuhakikisha kuwa Nchi mbili hizi zinafikia Malengo.
No comments :
Post a Comment