Mjumbe wa Kamati
Kuu ya Taifa ya Halmashauri kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mke wa Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Seif Ali Idi kwa kushiriki na
kufanikisha matembezi ya miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
wakati wa Ufungaji wa Matembezi ya Vijana wa CCM kuelekea kilele cha
Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika leo Januari
10,2020 katika Uwanja wa Mapinduzi SQuare Michenzani Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati
Kuu ya Taifa ya Halmashauri kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia suluhu Hassan, akihutubia Viongozi na
Vijana wa CCM mara baada ya kupokea Bendera na Picha mbalimbali za
Waasisi wa Taifa hili wakati wa Ufungaji wa Matembezi ya Vijana wa CCM
kuelekea kilele cha Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
yaliyofanyika leo Januari 10,2020 katika Uwanja wa Mapinduzi SQuare
Michenzani Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati
Kuu ya Taifa ya Halmashauri kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia suluhu Hassan, akipokea Bendera ya
Mapinduzi ya Zanzibar kutoka kwa Daud Kalela mmoja kati ya Vijana
Walioshiriki Matembezi ya Vijana wa CCM kuelekea kilele cha Miaka 56 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakati wa Upokeaji na Ufunguaji wa
Matembezi hayo yaliyofanyika leo Januari 10,2020 katika Uwanja wa
Mapinduzi SQuare Michenzani Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati
Kuu ya Taifa ya Halmashauri kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Msanii
kizazi kipya Asley kwenye Ufungaji wa matembezi ya Matembezi ya Vijana
wa CCM kuelekea kilele cha Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
yaliyofanyika leo Januari 10,2020 katika Uwanja wa Mapinduzi SQuare
Michenzani Zanzibar.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments :
Post a Comment