Baadhi ya Madiwani wa Hamashauri
ya Wilaya ya Sikonge wakiwa kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la
Sikonge la kujadili na kupitia mapendekezo ya makisio ya mapato na
matumizi ya mwaka 2020/21.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Martha Luleka akitoa ufafanuzi jana kwa
Madiwani kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la Sikonge la kujadili na
kupitia mapendekezo ya makisio ya mapato na matumizi ya mwaka 2020/21.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Peter Nzalalila akifungua jana mkutano
wa Baraza la Madiwani la Sikonge la kujadili na kupitia mapendekezo ya
makisio ya mapato na matumizi ya mwaka 2020/21.
Mbunge wa Sikonge Joseph
Kakunda akichangia hoja wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani la
Sikonge la kujadili na kupitia mapendekezo ya makisio ya mapato na
matumizi ya mwaka 2020/21.
…………………………………………………
NA TIGANYA VINCENT
Madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Sikonge wamewaagiza Afisa Utumishi na Mganga Mkuu wa Wilaya
(DMO) kuwachukua hatua Wauguzi wote walisababishia baadhi ya wakinamama
kujifungulia mapokezi wakiwa wanasubiri huduma.
Azimio hilo limetolewa jana na
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la
Sikonge la kujadili na kupitia mapendekezo ya makisio ya mapato na
matumizi ya mwaka 2020/21 baada ya baadhi ya Madiwani kulalamikia uzembe
wa wauguzi ulisababisha baadhi ya wanawake kujifungua bila msaada wa
Muunguzi.
Alisema ni vema wawaonyeshe hatua
mbalimbali walizowachukulia Wauguzi wa Zahanati ya Kirumbi, Kisanga na
Lembeli na watumishi walevi nyakati za kazi na Baraza la Madiwani
lipatiwe taarifa.
Nzalalila alisema kama
watashindwa kuwachukulia hatua itabidi Baraza limchukulie hatua Afisa
Utumishi na Mganga mkuu wa Wilaya ya kushindwa kuwasimamia watumishi
waliochini yao.
Awali Diwani wa kata ya Kipanga
Upendo Mgombozi alisema mama mmoja mjamzito alilazimika kujifungulia
mapokezi baada ya Muuguzi wa Zamu kudai hawezi kwenda kumsaidia kwa
sababu ya hali aliyonayo kiafya.
Alisema mama huyo alijifungua
mbele ya mume wake akiwa hana msaada wa Muuguzi yoyote na kuongeza kuwa
angaweza hata kupoteza maisha kwa sababu ya kutokuwa na msaada wa
mtaalamu.
Diwani huyo aliongeza kuwa hata
alipomwita katika Kamati ya Kata kwa ajili ya kumuonya alishikiria
msimamo wake kwamba asingeweza kumsaidia mama yule kwa sababu ya hali
aliyokuwa nayo siku ile.
Akijibu hoja za Madiwani Kaimu
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Dkt. Peter Songoro alisema baadhi ya
wauguzi waliozembea na kusababisha baadhi ya wanawake kujifungia wakiwa
wanagonja huduma wameshapewa onyo na Muuguzi mwingine tuhuma zake
zinaendelea kufanyiwa kazi na itakapokamilika watatoa taaifa ya hatua
waliomchukulia.
Aliongeza kuwa Zahanati hazipaswi
kufungwa bali zinatakiwa kufanyakazi saa 24 kila siku na kunakuwepo kwa
mtumishi wa zamu kulingana na mpango kazi na ratiba ya zamu
waliojipangia.
Aidha Dkt. Songoro aliwaomba Madiwani kuwahamasisha wananchi kushiriki katika ulinzi wa Zahanati katika maeneo yao.
Alisema kuwa Zahanati hizo zina
miliki vifaa vya gharama kubwa na kunapokuwa hakuna ulinzi inasababisha
hatari ya kupotea na wakati mwingine nyakati za usiku inasababisha
maisha ya watu ambao wengine wanakaa mbali na Zahanati kuwa hatarini.
No comments :
Post a Comment