N
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akimkabidhi Hati ya Kimila mmoja wa wananchi wa kijiji cha Litoa wakati wa
zoezi la kutoa hati lililofanyika kijiji cha Litoa wilayani Songea vijijini
mkoani Ruvuma jana. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti Mgema
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Hati ya Kimila Bibi Dafrosa Komba wakati
wa zoezi la kutoa hati kwa wakulima wadogo wa kijiji cha Litoa katika wilaya ya
Songea vijijini mkoani Ruvuma jana. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Songea
Pololeti Mgema.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Litoa katika wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma wakati
alipoenda kutoa hati za kimila katika kijiji hicho jana. Wa pili kushoto ni
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti Mgema.
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti Mgema akizungumza wakati wa zoezi la utoaji
Hati za Kimila kwa wakulima wadogo wa kijiji cha Litoa wilaya ya Songea
Vijijini mkoa wa Ruvuma uliofanywa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Dkt Angeline Mabula jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wananchi
waliokabidhiwa Hati za Kimila wakati wa zoezi la kutoa hati katika kijiji cha
Litoa wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti Mgema.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akielekea kukagua mradi wa
ujenzi wa nyumba na ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unaofanywa
na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika shamba la miti la Mpepo lililopo wilaya
ya Nyasa mkoani Ruvuma
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiangalia nondo zinazotumika kwenye ujenzi wa mradi
wa nyumba na ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unaotekelezwa
na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika
eneo la Mpepo wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma jana wakati akikagua mradi huo.
Kulia ni mhandisi wa Mradi kutoka NHC
Omar Chitawala.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akifafanua jambo wakati
akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba na Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS) unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwenye shamba la
miti la Mpepo lililopo wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma jana. Kushoto ni Meneja
Mawasiliano wa NHC Muungano Saguya na aliyekunja mikono ni Mhandisi wa Mradi
kutoka Omar Chitawala.Na Munir Shemweta, WANMM SONGEA
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekabidhi hati mia moja za
Kimila kwa wakulima wadogo wa kijiji cha Litoa kilichopo katika jimbo la
Peramiho wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma na kuwataka wamiliki wake
kuzitunza na kuzitumia hati hizo kujiletea maendeleo.
Akizungumza wakati wa
kuwakabidhi hati hizo katika kijiji cha Litoa wilaya ya Songea vijijini akiwa kwenye
shughuli za kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na miradi ya ujenzi ya
Shirika la Nyumba la Taifa katika mikoa ya kusini jana, Naibu Waziri Mabula
aliwataka wakulima waliokabidhiwa hati kutouza ardhi zao kwa nia ya kupata
fedha za haraka.
‘’Mmepiwa msikimbilie
kuuza ardhi bila kufuata taratibu kwa tamaa ya kupata fedha za haraka maana
mkiuza mnaweza kupunjwa fedha’’ alisema Dkt Mabula.
Aidha, Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha
zinaandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji ili kuwa na salama za miliki
za ardhi zilizoainisha maeneo ya shule, soko, maeneo ya kuabudia, viwanja vya
michezo pamoja na maeneo ya uwekezaji.
Dkt Mabula alizitaka pia halmashauri
kuandaa maeneo ya uwekezaji sambamba na kuhaulisha maeneo ili kuwa rahisi kwa
Mwekezaji atakayekuja kuwekeza katika sekta mbalimbali na kusisitiza kuwa ili
kuwaendeleza wananchi kiuchumi ni lazima ardhi ipimwe na kufanyiwa mpango wa
matumizi bora ya ardhi.
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Songea Vijijini Pololeti Mgema aliupongeza Mtandao wa Vikundi vya
Wakulima Tanzania (MVIWATA) kwa juhudi kubwa iliyofanya kufanikisha wakulima
wadogo kupata hati miliki za kimila na kubainisha kuwa wilaya yake imejifunza
bila kushirikisha wadau zoezi la kuwapatia hati wakulima wadogo lingechukua
muda mrefu.
Naye Mratibu wa MVIWATA katika mkoa wa Ruvuma
Laila Haji alisema Asasi yake iliona umuhimu wa wakulima wadogo kuwa na salama
za miliki za mashamba yao na ndiyo maana ikafanya juhudi kwa kushirikiana na
halmashauri ya wilaya ya Songea ili kuwapatia hati wakulima wa kijiji cha
Litoa.
Hata hivyo, alisema
changamoto kubwa iliyopo kwa wakulima na wananchi kwa ujumla katika suala la
hati miliki za ardhi ni elimu ndogo kuhusiana na masuala hati za ardhi, mfumo
dume kwa wanawake kumiliki ardhi pamoja na migogoro ya wakulima na wafugaji.
Katika
hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alitembelea mradi wa ujenzi wa Ofisi na
nyumba za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) uliopo Mpepo wilayani Nyasa
mkoa wa Ruvuma. Mradi huo pamoja na miradi mingine ya ujenzi wa nyumba na ofisi
za TFS katika maeneo mbalimbali nchini unajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC).
No comments :
Post a Comment