Katika
siku za hivi karibuni huduma ya kutuma fedha, kupokea na kulipa kupitia
simu za mkononi imekuwa jambo kubwa nchini na kwa kiasi kikubwa kichocheo cha maendeleo yetu.
simu za mkononi imekuwa jambo kubwa nchini na kwa kiasi kikubwa kichocheo cha maendeleo yetu.
Tafiti
nyingi zinaonyesha kuwa faida zinazohusiana na huduma za kifedha kwa
njia ya simu za mkononi zinachangia sana kwenye kubadilisha nchi yetu
kidijitali na kutusaidia kufikia malengo ya maendeleo kuelekea mwaka
2025.
Huduma
hii imewezesha watu wengi zaidi katika mfumo rasmi wa kifedha
(financial inclusion). Imewapa njia rahisi na ya hakika wananchi wa
kawaida na biashara kuweka akiba, kuwekeza, kutuma, kutoa na huduma
nyingine lukuki ambazo sote sasa tunazitumia kidijitali. Kwa
wafanyabiashara wadogo na wakati imewasaidia kukua zaidi, kukuza mtaji
na kuongeza uwekezaji na ajira.
Licha
ya maendeleo haya, bado wako ambao huduma hizi rasmi za kifedha na
mitaji hazijawafikia. Hatua inayofuata sasa ni kuhakikisha wale wote
ambao hawajafikiwa na matunda haya ya maendeleo nao wanayapata na huduma
ya fedha kwa njia ya simu ni njia muhimu na kuu zaidi kufikia watu
hawa.
Kukua
zaidi kwa huduma hii kunategemea msingi mzuri wa uwekezaji katika sekta
ya mawasiliano ya simu na mazingira mazuri ya kufanya biashara.
Tuungane
pamoja kuendelea kuipa nguvu sekta ya mawasiliano ya simu ili iendelee
kutanuka zaidi ili sote tufaidi matunda yake. Miezi michache iliyopita
kampuni mbili za Tigo na Zantel zimeunganisha shughuli zao.
Hii
ni hatua mojawapo ya kuboresha soko na kutoa huduma bora zaidi kwa
taifa. Tukianza mwaka huu mpya wa 2020 tuendelee kutumaini kwamba sekta
hii itaendelea kuwa bunifu ili kusukuma mbele dira ya maendeleo ya nchi
kuelekea mwaka 2025.
No comments :
Post a Comment