Moja ya mashine za Radiolojia za vipimo vya MRI zilizopo Hospitali za Serikali hapa Nchini.
Na Andrew Chale, Arusha
HOSPITALI
ya Rufaa ya Mount Meru, mkoani hapa ina mpango wa kuanzisha huduma za
vipimo vya MRI na CT-Scan ili kusogeza huduma hizo karibu na wananchi.
Akizungumza
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Shafii Msechu, wakati
akizungumza na waandishi wa habari na maofisa mawasiliano wa taasisi
zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, katika kampeni yake ya 'Tumeboresha Sekta ya Afya'.
Lengo la ziara hiyo ni kuangazia mafanikio ya Serikali yaliyopatikana katika sekta ya afya kwa kipindi cha miaka minne.
Alisema
miongoni mwa mipango ya Hospitali ni kuona huduma za kibingwa ikiwemo
vipimo hivyo vya MRI na TC- scan vinasogezwa karibu.
"MRI
na TC-Scan ni vipimo vya gharama. Huduma hizi kwa sasa hakuna na
zinatolewa nje ya hapa. Mpango ni kuwa na mashine hizi na kutoa huduma
karibu na wananchi ilikuwapunguzia gharama za kufuata mbali" alisema
Dkt. Msechu.
Huduma hiyo kwa sasa inatolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC.
Dkt. Msechu aliongeza kuwa wapo mbioni kuanzisha huduma za usafishaji wa figo.
Huduma hiyo inatarajiwa kuanza mra baada ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo litakalogharimu Sh. millioni 600.
Kwa
sasa upimaji wa eneo la ujenzi wa jengo la kutolea huduma hiyo,
umekamilika na wanasubiri fedha kutoka Serikali ili kuanza ujenzi huo.
"Hospitali
ya Mount Meru inatarajia kuanza kutoa huduma za usafishaji wa figo na
tayari tuna mashine tano za kuanza kutoa huduma hii tulizopewa na Wizara
na wadau wa afya na tunachosubiri ni fedha za kuanza ujenzi," alisema
Dkt. Msechu.
Alibainisha
kuwa, kuanzisha huduma hiyo ni kutokana na kuwapo kwa wagonjwa wenye
matatizo hayo lakini kutokana na kutokuwa na huduma hiyo wamekuwa
wakiwapeleka hospitali nyingine.
Dk.
Msechu alisema kwa mwezi wanapokea wagonjwa watatu wa Figo
wanawahamishia katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC.
Hospitali
hiyo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali za matibabu huku kwa siku
wanapokea wagonjwa wapya 320 hadi 500, wa marudio 250 hadi 350 na watoto
30 hadi 50.
Pia wana Madaktari bingwa wa kufanya upasuaji na asilimia 34 wanawafanyiwa wajawazito ambao idadi yao ni 200 kila mwezi.
Kadhalika alisema wanatoa msamaha wa matibabu ya wagonjwa 3,224 kwa mwezi na wanagharamia Sh. milioni 41.8.

No comments :
Post a Comment