Mwanafunzi wa shule ya sekondari
ya wavula FEZA Bw.Mvano Cabangoh akiwa pembeni na mama yake akiongea na
wanahabari baada ya matokeo ya kidato cha nne kutangazwa wakati yeye
akifanikiwa kushika nafasi ya sita kitaifa.
Mwanafunzi wa shule ya sekondari
ya FEZA BOYS Bw.Mvano Cabangoh(aliebebwa juu) akishangiliwa na baadhi ya
wanafunzi wenzake wa FEZA BOYS baada ya kutangazwa matokeo ya kidato
cha nne wakati kwa upande wake akishika nafasi ya sita kitaifa.
Mkuu wa shule za FEZA nchini
Bw.Ibrahim Yunus akiongea na wanahabari Jijini Dar es Salaam, baada ya
kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne nchini wakati shule ya FEZA
BOYS ikishika nafasi ya tatu Kitaifa.
*********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Uongozi wa shule za FEZA hapa
nchini umefurahishwa na matokeo yaliyotoka hasa baada ya
kufanya vizuri
katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne.
FEZA Boys imefanikiwa kushika
nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne wakati kwa
upande wa wanafunzi shule hiyo imetoa mwanafunzi mmoja ambaye ameshika
nafasi ya sita kitaifa.
Akizungumza na wanahabari jijini
Dar es Salaam, Mkuu wa shule za FEZA nchini Bw.Ibrahim Yunus amesema
kuwa jitihada za pamoja ambazo zilikuwa zinafanywa na walimu, wanafunzi
pamoja na wazazi ndizo chanzo cha shule hiyo kufanya vizuri kwenye
matokeo ya mitihani ya kitaifa.
“Lengo la shule za FEZA kuweza
kutoa elimu iliyobora kwa watanzania hasahasa tunazingatia tunakoelekea
katika uchumi wa viwanda hivyo masomo ya sayansi tunayapa kipaumbele ili
yaje yatujengee taifa letu”. Amesema Bw.Yunus.
Aidha, Bw.Yunus ametoa shukrani kwa wadau wote ambao wamewezesha elimu inayotolewa na shule hizo kuwa bora.
Kwa upande wa mwanafunzi ambaye
amefanikiwa kushika nafasi ya sita kitaifa Bw.Mvano Cabangoh amesema
kuwa siri ya kufanya vizuri katika mitihani yake ni pamoja na juhudi
ambazo alikuwa anazifanya hasa kupangilia ratiba zisizombana kujisomea
na muda wa kupumzika na kufanya mambo mengine pamoja na juhudi za wazazi
na walimu katika ufundishaji.
“Sikutegemea kama naweza kushika
nafasi hii ambayo nimepata maana kuingia katika kumi bora si rahisi kuna
wanafunzi wengi nchi nzima hivyo ilikuwa ni ngumu sana kuingia kumi
bora”.Amesema Bw.Cabangoh.
No comments :
Post a Comment