Na Mwandishi Wetu, Dodoma
NAIBU
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, ameagiza mfumo wa ushirika wa
stakabadhi ghalani kuanza mara moja kutekelezwaji katika mikoa mitatu ya
Mwanza, Shinyanga na Tabora, kwa ununuzi wa mazao ya dengu choroko.
Aidha,
Bashe, ameitaka tume ya maendeleo ya ushirika nchini, kuitisha kikao
cha wadau wa kilimo kwa mikoa hiyo, kwa nia ya kutoa muongozo kabla ya
kuanza kutumika kwa mfumo wa Ushirika wa Stakabadhi Ghalani.
Agizo
la Naibu Waziri huyo limetolewa katika kikao na wadau wa masuala ya
ushirika, kwa mikoa hiyo, kilichofanyika mapema wiki iliyopota mjini
Dodoma.
Naibu
Waziri huyo pia alimuagiza Naibu Mrajis wa vyama vya ushirika nchini,
Charles Malunde, kutembelea mikoa hiyo kukutana na wakuu wa mikoa pampja
na kuzungumza na wadau, kwa nia ya kuliweka sawa jambo hilo.
Waziri
Bashe, alisema serikali imebaini kuwapo kwa kasoro mwaka jana, kuzuia
mfumo huo kwenye ununuzi wa mazao hayo, lakini pia aliamua kulifanyia
kazi kwa kina na ndio maana amefanya haraka kutoa maelekezo hayo.
Naibu
Waziri Bashe, alisema kuwa njia bora ya kumkwamua mkulima masikini wa
kijijini ni kutumiwa kwa mfumo wa ushirika, ambapo wanunuzi hukutanishwa
na kushindanishwa kwenye soko la pamoja.
“Kwa
mfano wanunuzi wa dengu na choroko, hujitokeza na kuandikishwa na
warajis waasaidizi, lakini pia mazao ya wakulima hukusanywa kwenye
maghala makuu, ambapo mnada huitishwa na wanunuzi kila mmoja hujinadi
kwa bei,” alisema
“Chini
ya utaratibu huo na kwa usimamizi wa karibu wa wizara yetu kupitia tume
ya maendeleo ya ushirika, wakulima hujikuta wakipata bei nzuri na hivyo
kufikia malengo ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kumsaidia
mkulima masikini,” alisema Bashe
Alisema
tayari wakulima wa mikoa hiyo walikuwa wakililia mfumo huo wa ushirika,
huku wakihoji sababu za kuzuhiliwa mikoa ya kanda ya ziwa na kuruhusiwa
mikoa ya kusini pekee.
“Ninachoweza
kusema hapa ni kwamba, twendeni tukawasaidie wakulima kupitia mfumo wa
stakabadhi ghaani, lakini pia serikali imejifunza kitu kutokana na hali
hiyo,” alisema Waziri Bashe.
Aliongeza
kusema kuwa kupitia mfumo huo wa ushirika, vyama vikuu vya ushirika vya
Nyanza na Shirecu vitapata nguvu ya kujiendesha na pia kufikia malengo
ya kufufua mitambo yao na viwanda vyao vya pamba.
Hata
hivyo, alipotafutwa kwa niia ya simu kuhusu hatua waliyofikia baada ya
agizo hilo la Waziri Bashe, Malunde, alisema kwa ufupi, Nitakupigia
baadaye, lakini alipotafutwa tena hakupokea simu wala kujibu ujumbe
mfupi wa maandishi.
Meneja
wa SHIRECU Ramadhan Hamis, alikiri kushiriki kikao hicho na kusema wao
sasa wanasubiri maelekezo kutoka kwa tume hiyo ya ushirika, iweze
kutekeleza maagizo ya Waziri.
“Kimsingi
huku tupo tayari kwa ajili ya utekelezaj, hao tume waliambiwa waje
kuongea na wakuu wa mikoa pamoja na wadau, kuhusu mchakato wa suala
hilo, lakini tunaona mambo yako kimya,” alisema Hamis.
Mbali
na kukutana na wadau hao, pia Waziri Bashe, aliiagiza tume hiyo kutoa
tangazo kupitia vyombo vya habari kuhusu utekelezaji wa sheria ya
ushirika na kuanza kutumiwa kwa mfumo huo kwa mazao ya dengu na choroklo
kwa mikoa hiyo, lakini pia kuruhusu kutumika kwa mfumo kwenye maeneo
mengine.
Mwenyekiti
wa Tume ya Ushirika nchini Dkt. Titus Kamani, alieleza kufurahishwa
kutokana na maamuzi ya Naibu Waziri Bashe, akisema hatua hiyo itasaidia
kumuondolewa hasara mkulima, iliyokuwa ikisababishwa na walanguzi wa
mazao vijijini waliokuwa wakitumiwa na makampuni yasiyohitaji ushirika.
Ushirika
ndio sauti ya wakulima wanyonge na kwa kauli hiyo ya Waziri Bashe,
tumefurahi kwamba tupo njia moja kwa nia ya kumsaidia mkulima huyu
masikini, apate bei nzuri ya mazao yake, badala ya kuruhusu walanguzi
kuendelea kuwalaghai huko vijijni.

No comments :
Post a Comment