Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Christopher
Derek wakiangalia Gwaride la vikosi vya
ulinzi na usalama nchini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sherehe Uhuru kwa
mwaka 2019.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na wajumbe wa kamati ya maandilizi
ya Sherehe ya Uhuru zitakazofanyika Kitaifa Mkoa wa Mwanza wakiwasili kwa ajili
ya Ukaguzi wa Uwanja wa CCM Kilumba utakaotumika kwa ajili ya sherehe hizo.Alitembelea
tarehe 30 Novemba 2019.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wajumbe wa Jeshi la Jadi
(Sungusungu) alipowatembelea Novemba 30, 2019 kukagua maandalizi ya onesho
maalum linalohusu shughuli za ulinzi na amani wanazofanya ambalo litaoneshwa
wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za miaka 58 ya Uhuru, Jeshi hilo lipo Wilaya
ya Kwimba mkoani Mwanza.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Afisa Maadhimishi kutoka
ofisi yake, Bw.Stephen Magoha alipowasili katika Kijiji cha Hunghumalwa
Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza ili kukagua jeshi la jadi (sungusungu)
walioandaliwa kwa ajili ya kufanya onesho lao wakati wa kilele cha sherehe za
Uhuru (9 Desemba, 2019)
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mkuu wa itifaki Balozi Kanali
Wilbert Ibuge wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Kwimba apotembelea kukagua
maandalizi ya Jeshi la Jadi (Sungusungu) wanaoendelea na maandalizi ya onesho
maalumu katika sherehe za Uhuru mwaka huu.
Mkuu
wa Itifaki Balozi Kanali Wilbert Ibuge akizungumza na Jeshi la Jadi (hawapo
pichani) wanaoendelea na maandalizi ya onesho maalumu katika sherehe za Uhuru
mwaka huu mkoani Mwanza.
Mkuu
wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga na Mtemi wa Sungusungu wa Wilaya hiyo Bw.
Mogan Shimbi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu,
Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa
ziara yake kukagua maandalizi ya onesho maalum la sungusungu katika wilaya hiyo.
Sehemu
ya wajumbe walioshiriki kukagua onesho la sungusungu Wilaya ya Kwimba (hawapo
pichani) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimishi ya miaka 58 ya Uhuru kwa
mwaka 2019.
Sehemu
ya wajumbe walioshiriki kukagua onesho la sungusungu Wilaya ya Kwimba (hawapo
pichani) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimishi ya miaka 58 ya Uhuru
Baadhi
ya wajumbe wa Jeshi la Jadi (sungusungu) wakiimba mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama pamoja na viongozi alioambatana nao wakati wa ukaguzi wa
maandalizi ya Maadhimishi ya 9 Desemba, 2019 mkoani Mwanza.
Mtemi
wa Sungusungu wa Wilaya Kwimba mkoani Mwanza Bw.Mogan Shimbi akiwaongoza
wajumbe wa jeshi hilo kuimba wimbo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya onesho lao
la Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na wajumbe wa kamati ya maandilizi ya
Sherehe ya Uhuru wa Mkoa wa Mwanza wakiangalia maandalizi ya Gwaride la vikosi
vya ulinzi na usalama nchini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sherehe hizo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)NA.MWANDISHI WETU
Maandalizi ya
maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru yamefikia hatua za kuridhisha huku Serikali
ikieleza kuwa sherehe hiyo itapambwa na onesho maalum la Jeshi la Jadi la
sungusungu kutoka Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameeleza itakuwa ni mara ya kwanza kwa
jeshi hilo kuonesha namna wanavyofanya kazi za ulinzi katika maeneo yao ili
kuendelea kuenzi nia ya Rais wa Awamu ya Tano Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ya
kuilinda amani na utulivu uliopo nchini.
Waziri alieleza
hayo mapema Novemba 30, 2019 alipotembelea na kukagua maandalzii ya onesho hilo
yanayoendelea katika Kijiji cha Hunghumalwa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
“Hii itakuwa ni
mara ya kwanza kuwa na onesho hili maalum ambalo linatukumbusha nia ya Mhe.
Rais ya kuilinda amani iliyopo na kuhakikisha haichezewi kwa gharama yoyote na
kuona namna tunavyojivunia jeshi hili lililoundwa katika misingi na maadili
mema ya amani na utulivu,” alisema waziri Mhagama
Aliongezea
kuwa, Jeshi hilo litajumuisha zaidi ya sungusungu 1300 watakaoshiriki kwa siku
hiyo kwa kuongozwa na Manji wao pamoja na Mtemi wa Wilaya Mogan Shimbi.
Sambamba na
hilo maandalizi mengine ikiwemo, uandaaji wa uwanja wa CCM Kilumba, mazoezi ya
Majeshi (Gwaride), Usafi wa mazingira pamoja na vikundi vya burudani
yanaendelea mkoani hapo.
“Maandalizi
muhimu ikiwa ni pamoja na marekebisho ya miundombinu katika uwanja yanaendelea
pamoja na maandalizi muhimu ikiwemo, kutoa mialiko, kuandaa malazi kwa wageni, kuandaa vikundi vya ngoma
za asili, kuandaa gwaride , kuandaa wanafunzi wa watakaoumba umbo la bendera,
pamoja na nyimbo za kizazi kipya na mahitaji
mengine muhimu yapo katika hatua za kuridhisha,” alisema Waziri Mhagama
Aidha, kutakuwa
na vikundi vya burudani ikiwemo; ngoma za asili kutoka mkoa wa Mara (Ritungu)
na mkoa wa Mwanza, wimbo maalum kutoka Zanzibar pamoja na kwaya ya AIC Mwanza
na bendi ya Tanzania One Theatre (T.O.T) vitatumbuiza.
Alifafanua kuwa
maonyesho hayo yatakayofanyika Desemba 9 yatajumuisha gwaride maalumu la
heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama nchini.
“Watoto 3200 kutoka shule za msingi na sekondari
za mkoa wa Mwanza wataonesha umbo la bendera ya Taifa letu,” alisema Waziri
Mhagama
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella aliwasihi Watanzania kumuunga mkono
Rais Magufuli kwa kuendelea kuilinda amani iliyopo kwa kuzingatia kaulimbiu ya
mwaka huu pamoja na kuendelea kuwa na uzalendo na kufanya kazi kwa bidiii kwa
ajili ya kujiletea maendeleo.
Pia, aliwataka
wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo na kuendelea kujiandaa
kwa bidii, usanifu na ubunifu wa kipekee katika kuiadhimisha siku hiyo muhimu.
“Ninamshukuru
sana Mhe. Rais kwa kuelekeza maadhimisho haya kufanyika mkoani kwetu, niiwaase
wananchi wa Mwanza kuitumia heshima tuliyopewa kwa kujitokeza kwa wingi katika
siku hiyo ili kuunga mkono jituhada za Mhe. Rais wetu,” Alisisitiza Mongella
Sherehe za Maadhimisho
ya Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri kwa mwaka huu (2019) kitaifa
yatafanyika Mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kilumba ambapo Mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli na kupambwa na kauli mbiu inayosema “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na
Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Tifa letu”
No comments :
Post a Comment