Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Nguruka katika mkutano wa hadhari uliofanyika kijiji humo.
Wananchi wa Nguruka wakimsikiliza
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani wakati akihutubia kwenye mkutano
wa hadhari uliofanyika kijiji humo.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani(katikati) akitoa magizo
kwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko ( kushoto) ya
kuwachukulia hatua wakandarasi wa kampuni ya ETERN-CCCE baada ya
kutoridhishwa na utendaji kazi wao.
*****************************
Hafsa omar-Kigoma
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani ametoa agizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua
Mrindoko kuwaweka ndani na kuwanyang’anya pasipoti zao, wakandarasi wa
kampuni ya ETERN-CCCE waliopewa kazi ya kusambaza umeme vijijini baada
ya kusuasua katika utekelezaji wa kazi.
Alitoa agizo hilo Desemba 22,2019,
akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nguruka,
Wilaya ya Uvinza, Mkoani Kigoma, katika ziara ya kazi kukagua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme mkoani humo.
Aidha, alisema amechukua hatua
hiyo mara baada ya kukagua kazi ya usambazaji umeme Mkoani humo na kuona
maeneo mengi yakiwa bado hayajasambaziwa umeme kutokana na kusuasu
katika kazi kwa mkandarasi huyo.
“ Wameanza kazi lakini spidi yao
ni ya kusuasua sana, spidi yao hairidhishi huo ndio ukweli, lakini
hatuwezi kubaki tunalalamika lazima tuanze kuchukua hatua, leo nimekuja
kukagua hapa nimekuta amewasha vijiji saba tu ambapo zaidi ya vijiji
hamsini bado havijawashwa ” alisema.
Dkt. Kalemani, pia alichukizwa na
kitendo cha wakandarasi hao kufanya kazi kwa udanganyifu kwa kuweka
nguzo na transfoma katika eneo hilo siku moja kabda ya ziara yake
kijijini humo, na kuwataka wakandarasi hao kufanya kwa mujibu wa
mkataba.
Vile vile, aliwagiza wakandarasi
hao ifikapo januari 10 mwakani wawe tayari wamewasha umeme katika kijiji
hicho na Vitongoji vyake vyote na kuongeza spidi ya kufanya kazi pamoja
kuajiri vibarua wengi ili kasi ya usambazaji umeme iongezeke.
Katika ziara yake mkoani humo,
Waziri wa Nishati, alikagua ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha
Nguruka, kituo ambacho kikikamilika Mkoa wa Kigoma utaunganishwa na
gridi ya taifa.
No comments :
Post a Comment