| Wafanyakazi wa TTCL Corporation wakiwa katika zoezi la kuchangia damu kwenye kituo cha damu cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo jijini Dar es Salaam. |
| Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Bw. Waziri Kindamba akichangia damu katika kituo cha damu cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo jijini Dar es Salaam. |
Na Mwandishi Wetu
WAFANYAKAZI wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Bw. Waziri Kindamba leo wamejitokeza kuchangia damu katika kituo cha damu cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
WAFANYAKAZI wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Bw. Waziri Kindamba leo wamejitokeza kuchangia damu katika kituo cha damu cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Akizungumza katika zoezi hilo
Mkurugenzi Mkuu, Kindamba alisema TTCL kwa mwaka huu imeona isherehekee
kwa namna tofauti kwa Shirika kupitia Wafanyakazi wake kutoa zawadi ya
kuchangia damu, tukio linaloonesha upendo wa kipekee katika kuokoa
maisha ya ndugu, jamaa na Watanzania wote waitaji.
Alisema msimu wa Krismasi ni wakati wa kuonesha upendo, kushukuru kwa mambo mengi ambayo yamepita katika mwaka mzima. Kindamba alibainisha kuwa TTCL inaamini kuwa damu waliochangia itaenda kuziba pengo la uhitaji katika benki ya damu MNH, na pia kuokoa maisha ya baadhi ya Watanzania.
Alisema msimu wa Krismasi ni wakati wa kuonesha upendo, kushukuru kwa mambo mengi ambayo yamepita katika mwaka mzima. Kindamba alibainisha kuwa TTCL inaamini kuwa damu waliochangia itaenda kuziba pengo la uhitaji katika benki ya damu MNH, na pia kuokoa maisha ya baadhi ya Watanzania.
“Ni vyema tukatambua kuwa
kuchangia damu si tu kwamba ni suala la kibinadamu katika kusaidia watu,
bali pia ni thawabu kubwa kwa Mwenyenzi Mungu. Tafiti mbalimbali
zinaonesha watu walio katika uhitaji wa damu ni pamoja na Mama
Wajawazito, Watoto, Wagonjwa wa upasuaji na wahanga wa ajali za moto na
barabarani. Hivyo tumetambua hili na kuzingatia kuwa yawezekana tukawa
wahanga siku moja na kuhitaji huduma ya damu,” alisema Kindamba.
Aidha aliongeza kuwa TTCL
Corporation inachukulia tukio hilo kama sehemu ya huduma kwa jamii,
ambayo Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation linajisikia
fahari kuitoa na kuihudumia jamii, hivyo kutoa rai kwa Watanzania wote
kujitokeza kuunga mkono juhudi za kuchangia damu.
“Nipende kutumia nafasi hii
kuihamasisha jamii na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali
kuweka utaratibu wa kuchangia damu kwani janga kubwa la kibinadamu kwa
sasa ni upungufu mkubwa wa upatikanaji wa damu salama na kwa wakati
muafaka,” alisisitiza Mkurugenzi Kindamba.
Kwa upande wake, Afisa
Muhamasishaji Damu Muhimbili, John Daniel Bigambalaye amewapongeza
wafanyakazi wa TTCL kujitokeza kuchangia damu kwa hiyari hivyo kuwaomba
mashirika mengine na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kuchangia damu.
| Baadhi ya Wafanyakazi wa TTCL Corporation wakichangia damu kwenye kituo cha damu cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo jijini Dar es Salaam. |
Alisema uhitaji wa damu Hospitali
ya Taifa Muhimbili ni mkubwa na damu haitengenezwi popote zaidi ya
kuomba kwa raia wenye afya njema kujitokeza na kuchangia damu. Alisema
takribani chupa 200 za damu hutumika kwa siku katika hospitali hiyo
kuokoa maisha ya wahitaji hivyo kuomba Watanzania kujitokeza kuchangia
damu ili kuokoa maisha ya wahitaji.
“Ni jukumu letu sote kubeba
dhamana ya kuokoa maisha ya wenzetu na ya kwetu wenyewe kwakuwa mstari
wa mbele kuchangia damu ili kuhakikisha watu wa rika zote wanapata fursa
ya damu kwa gharama nafuu na kwa wakati,” alisema Bigambalaye.
No comments :
Post a Comment