Madaktari bingwa wa magonjwa ya
moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao
kutoka King Salman Humanitarian Aid and Relief Center wa nchini Saud
Arabia wakimfanyia upasuaji wa bila kufungua kifua na kuziba tundu la
moyo wa mtoto kwa kutumia mtambo wa Cathlab wakati wa kambi maalum ya
matibabu inayofanyika katika Taasisi hiyo. Jumla ya watoto 33
wamefanyiwa upasuaji mdogo wa bila kufungua kifua ambapo hali zao
zinaendelea vizuri na wengine wameruhusiwa kurudi nyumbani.
Madaktari bingwa
wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
kwa kushirikiana na wenzao kutoka King Salman Humanitarian Aid and
Relief Center wa nchini Saud Arabia wakimfanyia mtoto upasuaji mkubwa
wa kusimamisha moyo na kurekebisha mishipa ya damu ya
moyo katika kambi maalum ya matibabu inayoendelea katika Taasisi hiyo.
Jumla ya watoto 23 wenye matatizo ya moyo wamefanyiwa upasuaji mkubwa
na hali zao zinaendelea vizuri.
Picha na JKCI
No comments :
Post a Comment