Mkurugenzi wa JK Cement Amit
Kothari akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Hyatt jijini
Dar es salaam leo mara baada ya kuingia makubaliano ya kibiashara na
kampuni ya Gold Star ya jijini Dar es salaam.
Baadhi ya watendaji wa kampuni hizo wakiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa JK Cement Amit
Kothari akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Goldstar Bw. Srinivasan
mara baada ya kusaini makubaliana ya kibiashara jijini Dar es salaam leo
Kulia ni Pushpendra Singh.
Picha ya pamoja.
……………………………………
DIRA ya Serikali ya awamu ya tano
ambayo imejikita katika ujenzi wa viwanda imezidi kuwavutia wawekezaji
wengi zaidi wenye uhitaji wa kuwekeza na kutengeneza masoko zaidi
nchini, ambapo leo Desemba 05 kampuni ya JK White cement (Afrika)
Limited ambayo ni
sehemu ya kampuni ya JK ya nchini India imetangaza
rasmi kuungana kibiashara na kampuni ya uzalishaji wa rangi ya Goldstar
Paints ya Tanzania ili kuingiza sokoni bidhaa mpya ya JK Wall Putty
bidhaa ambayo ni poda laini itokanayo na saruji nyeupe yenye kutoa
mwonekano mzuri kwa kuta na dari ambayo itaenda sambamba na mazingira.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa JK cement Amit Kothari amesema, ushirikiano huo wa
kibiashara umelenga kukata kiu ya wananchi kwa kutoa bidhaa bora yenye
kuendana na mazingira.
“JK Cement ni moja kati ya
wazalishaji bora wa cement na tumepata washirika Makini ambao tutaziba
ombwe lililopo pamoja na kutoa ajira, na kubwa zaidi ni kufungua ofisi
na kupandisha bendera Tanzania kwa mara ya kwanza katika ukanda wa
Afrika na dunia, na hiyo ni kutokana na ushirikiano mzuri tunaooneshwa
na Serikali ya Tanzania” ameeleza Kothari.
Amesema kuwa wanajivunia kuwa
sehemu ya watanzania na kueleza kuwa kampuni hiyo isiitwe ya wahindi
bali watanzania kwa kuwa Goldstar Paint wamekuwa kwenye safari na
dhamira ya kutoa bidhaa zenye ubora zenye kukidhi mahitaji ya watanzania
kupitia bidhaa zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Goldstar Srinivasan
amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele hasa katika masoko kwa
Kuhakikisha kwamba inaleta bidhaa zenye viwango stahiki na kwa sasa
wameongeza bidhaa nyingine kwenye soko jambo ambalo wanaamini litaleta
mabadiliko na mapinduzi katika kuwahudumia wateja.
Amesema kuwa JK ikiwa moja kati ya kampuni kubwa za uzalishaji
wa saruji nyeupe duniani na mzalishaji mkuu wa bidhaa ya Wall Putty
nchini India wataendelea kuwahudumia watanzania kwa kuwapa bidhaa bora
zaidi ambazo zinaendana na mazingira.
Kampuni ya JK cement yenye makazi yake Fujairah (UAE) wamekuwa
wadau kwa nchi za Afrika na katika kujipapanua zaidi wamejiegemeza zaidi
katika kukuza soko lake Tanzania kupitia muungano huo wa kibiashara na
kampuni ya Goldstar iliyoanzishwa mwaka 1988 wamekuwa maarufu zaidi
kupitia rangi ya Goldstar ambayo hupatikana kote nchini na ilichaguliwa
miongoni mwa makampuni 50 bora zaidi nchini na TBS na TPSF mwaka 2017.
No comments :
Post a Comment