TEMESA inapenda kukanusha uvumi
unaoenea mitandaoni kupitia video pamoja na picha zikielezea kusimama
kwa huduma za vivuko katika kivuko cha Kigongo Busisi mkoani
Mwanza
kutokana na kuwepo kwa magugu maji. Tukio la magugu maji lilitokea siku
ya tarehe 24 Desemba 2019 na magugu maji hayo yaliondolewa.
Shughuli za uvushaji abiria
zinaendelea kama kawaida katika kivuko cha Kigongo Busisi. TEMESA
inapenda kuwataarifu abiria wote waendelee kutumia huduma za kivuko
hicho kwakua kipo salama
Aidha TEMESA inawakumbusha abiria wote kuzingatia matangazo ya usalama yanayotolewa na mabaharia watumiapo vivuko.
Imetolewa na Kitengo cha Masoko Habari na Uhusiano kwa Umma TEMESA
No comments :
Post a Comment