Saturday, December 28, 2019

Mvua zinazoendelea kunyesha zazua tafrani shule Sombetini Mkoani Arusha



Katibu wa chama cha mapinduzi ccm bi zubeda abdalah akiwasisitiza wananchi watoke nje ili kuokoa maisha yao dhidi ya mafuriko  ambayo yametokea karibu na shule ya msingi sombetini picha na Queen lema Arusha.
*************************************
Na Queen Lema Arusha
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mvua zinaziendelea kunyesha jijini arusha zimesababisha maji kujaa katika shule ya msingi sombetini hali ambayo imesababisha viongozi mbalimbali wa
chama cha mapinduzi kutoa maji hayo
Akizungumza ndani ya shule hiyo ya sombetini katibu wa Uwt kata ya sombetini Bi Mwajaby Mvamba amesema kuwa mvua hizo zilianza kunyesha majira ya saa tisa na imeharibu miundombinu ya shule hiyo
Alisema kuwa wao kama viongozi wa chama wamelazimika kutoa maji ambayo yameharibu vibaya miundombinu ya shule hiyo ambayo wanafunnzi wanatarajia kufungua shule january 6 mwaka huu
“Maji ni mengi sana kwa kweli yamejaa sana na hata huenda hata taarifa mbalimbali zikaharibika ila tunapambana sana kuhakkisha madhara hayatokei kwa maslahi ya shule yetu”
Naye katibu wa Osunyai jr Zubeda Abdalah alisema kuwa wao kama wadau wa elimu wanaomba serikali kuboresha miunfombinu zaidi ya shule hasa hiyo ya sombetini
Zubeda alifafanua kuwa kwa masaa machache wamelazimika kuarisha kazi zao na kutoa maji ambayo yalikuws yamejaa katika shule hiyo ya sombetini na madarasa ambayo yamedhurika na maji hayo ni madarasa ya awali darasa la kwanza na darasa la pili.

No comments :

Post a Comment