
NA SULEIMAN MSUYA
KUNDI la
wanachama na washabiki Timu ya Simba maarufu ‘Simba Jamii’ limejipanga
kufanya ziara ya kutembelea vivutio vya utalii na kuvitangaza nchini na
nje ya nchi.
Hayo yamesemwa jana na Katibu wa Kundi hilo, Severine Kasimba “Chelsimba” wakati
akizungumza na gazeti jijini Dar es Salaam.
Kasimba
alisema ‘Simba Jamii’ imepania kufanya kazi ya kuielimisha jamii ya
Tanzania kupenda na kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili
kuongeza mapato kwa Serikali.
“Simba Jamii
tumekuwa tukihamasisha mambo yanayohusu timu yetu na tumefanikiwa kuwapa
wafuasi wengi, ila kwa sasa tunajipanga kuelekezanguvu zetu kwenye
kutangaza vivutio vya utalii na mapema mwakani tunatarajia kwenda
Hifadhi ya Taifa Saadan,” alisema.
Alisema kundi
hilo chini ya Mwenyekiti, Gabriel Ntole “Meneja Kijana” litatumia
wanakundi wake kuhakikisha sekta ya utalii inatangazwa.
Kasimba
alisema iwapo wao wakishirikiana na sekta nyingine ni sekta ya utalii
inaweza kupaa na kuongeza mapato mengi na kuchochea maendeleo.
Alisema Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyopo Bagamoyo ni sehemu pekee duniani ambayo ipo pembezoni mwa bahari.
Katibu huyo alisema mkakati mwingine wa ‘Simba Jamii’ ni kutangaza hifadhi mpya ya Burigi iliyopo Kanda ya Ziwa.
“Kwa sasa
wakati tukipanga taratibu za kuanza ziara hizo za kuitangaza na
kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kutembelea hifadhi zetu ili kuwa
mabalozi, pia tupo mbioni katika kuhimiza wanamichezo wote kushirikiana
nao na kuukuza utalii kwa kupitia sekta ya michezo,” alisema.
No comments :
Post a Comment