
*******************************
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
Kamanda wa polisi
mkoani Pwani, (ACP) Wankyo Nyigesa amesema ,mwaka 2019 makosa ya jinai
yamepungua kwa asilimia 10.5 na kuongeza kwamba hali ya usalama kijumla
ni shwari.
Aidha amesema, makosa
ya kukutwa na silaha na risasi walikamata jumla ya sila 17 ikiwa ni
pamoja na SMG moja na magobore 16 na risasi sita za SMG huku watuhumiwa
20 walifikishwa mahakamani kutokana na makosa hayo.
Aliweka bayana hayo
wakati akielezea namna walivyojipanga kudhibiti masuala ya uhalifu
wakati wa sikukuu ya krismas na mwaka mpya.
Wankyo, alieleza yaliyoripotiwa katika vituo vya
polisi ni 2,074 ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo makosa yalikuwa
2,318 hivyo yamepungua kwa makosa 244.
Alisema, kati ya
makosa hayo makosa ya jinai dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji ,kubaka
,kulawiti mwaka uliopita yalikuwa makosa 382 ,na mwaka huu yameripotiwa
makosa 366 hivyo yamepungua 16 sawa na asilimia 12.
“Makosa ya kuwania
mali kama vile unyang’anyi na kutumia silaha,unyang’anyi wa kutumia
nguvu ,wizi wa silaha ,uvunjaji nayo yamepungua makosa 236 sawa na
asilimia 19,kutoka makosa 1,240 mwaka 2018 hadi kufikia makosa 1,004
yalitokea mwaka huu”alifafanua.
Kamanda huyo
alibainisha, jeshi hilo pia lilizuia magendo na uhalifu katika bandari
bubu ,na kukweps ushuru zilikamatwa mafuta ya kupikia madumu 5,260
,khanga balo 16,matairi ya pikipiki 175, mafuta ya diezel lita 320
yalikamatwa huku watuhumiwa 23 walifikishwa mahakamani.
Hata hivyo
Wankyo,aliwataka wananchi washeherekee sikukuu kwa amani na utulivu na
kuyataka magari yasijaze abiria kupita kiasi na madereva wafuate sheria
za usalama barabarani pasipo kulewa wala kuendesha kwa mbwembwe.
Aliwaasa wamiliki wa kumbi za starehe, wasijaze watu kupita kiasi kwa matamanio ya kuongeza wateja ili kujipatia kipato.
No comments :
Post a Comment