Mgeni
rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (wa pili kulia)
akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano akiwa ameambatana na mwenyeji wake
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Godfrey Zambi (kushoto) pamoja na Katibu
Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge (kulia) wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika
katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi. Wengine katika
picha ni Mstahiki Meya wa Lindi mjini Ndugu Mohamed Liumbwe pamoja na
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Issa Ndemanga.
Katibu
Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge akitoa neno la ukaribisho kwa
wageni waalikwa na kutambulisha meza kuu wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika
hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Mh. Godfrey Zambi akitoa salamu kwa mgeni rasmi
pamoja na wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi
uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akizungumza na
wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuzindua wa Mwongozo wa fursa za
Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach
Resort mkoani Lindi.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dk.Tausi Kida Dk. Hoseana Lunogelo akitoa salamu za ESRF kwa
niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo wakati wa hafla ya kuzindua
wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika
hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mkuu
wa Ukuaji wa Maendeleo Jumishi na Mtaalamu wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Miradi ya Maendeleo (UNDP), Ernest Salla
akitoa salamu za UNDP kwa niaba ya Mwakilishi Mkaazi wa UNDP nchini
Tanzania.Bi. Christne Musisi wakati wa hafla ya kuzindua wa Mwongozo wa
fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea
View Beach Resort mkoani Lindi.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dk.Tausi Kida Dk. Hoseana Lunogelo akikabidhi Mwongozo wa fursa
za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
Mhe. Gelasius Byakanwa tayari kuzinduliwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa
mwongozo huo wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View
Beach Resort mkoani Lindi.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (wa pili kulia)
akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji
wa mkoa wa Lindi sambamba na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh.
Godfrey Zambi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo huo uliofanyika
katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi. Wanaoshuhudia tukio
hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Issa Ndemanga pamoja na
Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (katikati)
akionyesha nakala za Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi
mara baada ya kuzindua rasmi wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli
ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu
wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Issa Ndemanga, Katibu Tawala Mkoa wa
Lindi, Bi. Rehema Madenge Mstahiki Meya wa Lindi mjini Ndugu Mohamed
Liumbwe pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Issa Ndemanga.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akikabidhi nakala
ya Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi kwa Mkuu wa Ukuaji wa
Maendeleo Jumishi na Mtaalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Miradi ya Maendeleo (UNDP), Ernest Salla wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Mwongozo huo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi
uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akikabidhi nakala
ya Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi kwa Naibu Kamishna wa
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) – Utalii na Huduma
za Biashara Bw. Imani Nkuwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo huo
wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea
View Beach Resort mkoani Lindi.
Mtafiti
Mwandamizi wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo (kulia) pamoja na Mtafiti
mshiriki kutoka ESRF Musa Martine wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika
hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mwekezaji
wa hoteli za fukwe za bahari mkoani Lindi Bw. Sultan Ahmed kutoka Kilwa
akitoa ushuhuda kuhusu fursa zilizopo ndani ya mkoa wa Lindi wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi
uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya wageni waalikwa walioshiriki hafla ya
uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika
katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na meza kuu wakiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya za Lindi na Wilaya
za Mtwara wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji
wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort
mkoani Lindi.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na meza kuu wakiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau waliowekeza kwenye mkoa wa
Lindi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa
mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani
Lindi.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na meza kuu wakiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau kutoka ESRF, UNDP, Equinor,
Shell, taasisi mbalimbali za serikali na sekta binfasi wakati wa hafla
ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi
uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na meza kuu wakiwa
kwenye picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya mkoa wa Lindi wakati
wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi
uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Na Mwandishi Wetu, Lindi
MKOA
wa Lindi umezindua Mwongozo wa Uwekezaji mkoani humo ambao umeanisha
fursa za uwekezaji zilizopo Lindi ili kuvutia wawekezaji kwa lengo la
kukuza uchumi wa mkoa na kuimarisha pato la mtu mmoja mmoja na taifa.
Mwongozo huo umezinduliwa tarehe 27 Novemba 2019 na Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara, Gelasius Byakanwa.
Mwongozo
huo umeandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa
kushirikiana na wataalam wa Mkoa wa Lindi chini ya ufadhili wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Akizindua
mwongozo huo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa alitaka fursa
hizo zilioanishwa kutekelezwa kimkakati ili kuongeza kipato cha wananchi
na Mkoa wa Lindi.
Alisema
mkoa wa Lindi umefanyakazi kubwa ya kuongeza kilimo cha korosho na
ufuta na kusema hiyo ni fursa kubwa kama ilivyo katika utalii kutokana
na kuwa na misitu mingi ya hifadhi na fukwe nzuri zaidi za kitalii
nchini na duniani. Alisema inawezekana pia kuanzisha siku maalum ya kula
nyama pori wilayani Kilwa ili kuchochea utalii.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi M kuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey
Zambi alisema Kongamano la Biashara na Uwekezaji lililoandaliwa na Mkoa
kwa kushirikiana na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Machi mwaka
huu limeleta wawekezaji wa ndani na nje ya mkoa kuja kuwekeza katika
sekta mbalimbali.
Alisema
Chuo cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Salaam ni kati ya taasisi
zilizoonesha nia ya kuwekeza na kimepewa ekari 150 za ardhi bure kwa
ajili ya Chuo cha Kujenga Boti na Meli. Mwekezaji mwingine ni Sarah
Masasi anayetaka kujenga Kiwanda cha kubangua korosho na amepatiwa ekari
50 bure za ujenzi huo.
Alisema
kampuni ya kimataifa ya Norway inatarajia kuwekeza kituo cha sayansi,
ufugaji na kilimo na kampuni kutoka India kuwekeza kwenye uvuvi.
Hakutaja majina ya kampuni. Aidha kampuni kutoka Ujerumani, Filloship
inafanya mazungumzo kuwekeza mkoani hapa.
Katika
hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa,
kampuni za mafuta na gesi za Equinor, Shell, wakuu wa wilaya,
wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya na manispaa, taasisi za
umma, wawekezaji na sekta binafsi, Zambi alisema kutokana na kongamano
hilo walianzisha ofisi ya uratibu wa uwekezaji.
”Tunaishukuru
TSN (wachapishaji wa magazeti ya HabariLEO, Daily News na SpotiLeo)
kutufungulia mlango kupata wawekezaji Marekani, Ujerumani, India na
nchini,” alisema Zambi. Pia, aliwashukuru Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi
na Kijamii (ESRF) kwa kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Lindi.
Alisema
kuna miradi mikubwa ambayo inashughulikiwa na serikali kuu hapa mkoani
ikiwa ni pamoja na mradi wa kiwanda cha mbolea Kilwa. Mkoa una fursa ya
kuwa na kiwanda cha usindikaji chumvi, utengenezaji wa mvinyo kw
akutumia korosho, viwanda vya vifungashio, viwatilifu, kubangua korosho
na usindikaji wa mafuta ya nazi, alizeti, nishati mbadala nk.
Aidha
alisema kwamba fursa katika ngazi ya halmashauri ni pamoja na makundi
madogo ya wachambuaji korosho, misitu na utalii na pia kuongeza mnyororo
wa thamani katika bidhaa mbalimbali za Kilimo katika ngazi za wilaya na
halmashauri.
Alisema
kuna utajiri mkubwa wa urithi wa utamaduni na wanamatarajio taaaisi za
kitaifa kama Tawa zitasaidia kuwepo na utalii unaowezesha kuchangia kwa
kiasi kikubwa pato.
Katika
masuala ya uwekezaji katika utalii, mmoja wa wafanyabiashara mkoani
Lindi, Sultani Ahmed Sultani alizungumzia kwa kina katika mada yake
namna bora ya kuwezesha sekta ya utalii akitaka sekta binafsi kuwezeshwa
ili kushiriki katika nafasi hiyo.
Alisema
Lindi ina nafasi kubwa ya kuleta watalii kutoka kaskazini na Kusini mwa
Afrika kupitia mpango maalumu unaoweza kuungwa na Zanzibar na matunda
yake yataonekana.
Dkt.
Hoseana Lunogelo, Mtafiti Mwandamizi akizungumzia Mwongozo wa Uwekezaji
wa Mkoa wa Lindi kwa niaba ya Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi Mtendaji
Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), alisema watafiti wake
wameona fursa nyingi sana na ziko katika sekta na ngazi zote.
“Kwa
hapa Lindi fursa kubwa ipo kwenye mnyororo wa thamani wa zao la
Korosho, utalii na madini bila kuisahau gesi. Pia kuna fursa nyingi
katika Sekta ya Viwanda, Kilimo, Uvuvi, Miundombinu na Huduma. “ alisema
Dk Kida katika hotuba yake iliyosomwa na Dkt. Lunogelo.
Alisema fursa hizo zilizoainishwa katika mwongozo zikitumika vizuri zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha ya wananchi.
Mpaka
sasa ESRF imesaidia Mikoa 24 kuandaa Miongozo ya Uwekezaji ambapo mikoa
14 imekamilisha na Mikoa 10 iko katika hatua mbalimbali. ESRF tayari
imeanza kusaidia zoezi hili katika mikoa iliyobaki.
Naye
Bw. Ernest Salla akitoa neno kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Christine Musisi
ameisihi mikoa iliyokwisha tengenezewa miongozo kuhakikisha kwamba
wanafanyaia kazi miongozo hiyo ili kuleta tija.
Katika
hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Bw. Ernest Salla alisema
kwamba baada ya kuzinduliwa kwa amwongozo ipo haja kwa mkoa wa Lindi
sasa kuangalia vipaumbele na kuchambua vilivyotayari ili kuyafanyiakazi
kwa haraka.
Aidha
hatua nyingine ya pili ni kutangaza fursa zilizopo na kuandaa mikutano
ya uwekezaji kwa kuwakutanisha wawekezaji. Pia watumishi
wanaoshughulikia uwekezaji ni vyema wakaandaliwa kusaidia kusukuma mbele
gurudumu hilo na kutayarisha nyaraka mbalimbali kielektroniki ili kila
mmoja aweze kuzipata.
Pia
aligusia haja ya kuhakikisha fursa hizo zinatambuliwa kwa mabalozi
wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na mabalozi wetu nje ili kuuza fursa
hizo na kutafuta mitaji ili kuiwezesha sekta binafsi inashiriki
kikamilifu.
Mwakilishi
Mkazi wa UNDP alisema shirika lake litaendelea kushirikiana na Serikali
ya Tanzania na ESRF katika kuhakikisha kwamba wanakamilisha kutengeneza
Miongozi kwa mikoa iliyobaki.
No comments :
Post a Comment