Thursday, December 26, 2019

KAMPUNI YA L-VIC INVESTMENT LIMITED YAANZA KUTEKELEZA FURSA ZA KITALII KAGERA.



***********************************
Na Silvia Mchuruza.
Bukoba.
Mkurugenzi mtendaji Wa kampuni ya L-VIC investments limited  Bw. Anic Kashasha amesema kuwa  kagera ina fursa nyingi za kutosha lakini kampuni hiyo imekuja na mpango Wa Lake Victoria Basin Tourism Expo ambapo mpango huo utajadili  mnyororo Wa thamani katika fursa hiyo ya utalii.
Akizungumza na waandishi Wa habari Bw. Kashasha amesema kuwa wanakagera sasa hasa wale wanautalii wadogo watanufaika zaidi ikiwa mpango huo Wa Lake Victoria Basin Tourism Expo utajadiliwa katika kongamano litakalofanyika  katika ukumbi Wa ELCT Bukoba ikiwa lengo ni kujadili mnyororo Wa thamani kuhusu utalii pamoja na  hifadhi za taifa ambazo zimezinduliwa katika wilaya ya karagwe na kyerwa.
“Niseme tu kuwa wanakagera wachangamkie fursa zinazokuja kutokana na kupata hifadhi tatu za utalii kama burigi chato,Ibanda Kyerwa, na Rumanyika karagwe ambapo katika kungamano hili wawasilishaji Wa mada watakuwa ni tanapa lakini pia niseme kutakuwepo mada mbalimbali zinazohusu utalii” alisrma bw. Kashasha.
Hata hivyo amaeongeza kuwa kutakuwepo na wahusika wengi pamoja na wafanyabiashara hata waandaji Wa safari za utalii Wa utamaduni lakini pia watu Wa  CRDB kagera watakuwepo mamlaka ya mapato Tanzania pamoja na shirika la ndege ATCL zikiwemo na taasisi mbalimbali za serikali.
Sambamba na hayo amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa na mpango wa kuanzisha fursa ya utalii ya Lake Victoria Basin Tourism Expo ndani ya miaka zaidi ya mitano ambapo lengo kubwa zaidi ni kujadili fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta  ya utalii kagera na kuwataka wananchi pamoja na wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo.

No comments :

Post a Comment