Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
WANANCHI wa Mji wa
Kibaha ,mkoani Pwani wamehimizwa kupanda miti ya asili ambayo ipo
hatarini kutoweka pamoja na kulinda mazingira kwa faida na manufaa ya
kizazi kijacho.
Aidha wananchi wameaswa kuacha kukata miti na misitu ovyo kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha kuondoa uoto wa asili.
Rai hiyo ilitolewa na
mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la –
SAHO-linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti na kuhimiza kutunza
mazingira , Emmanuel Sago wakati wa zoezi la ugawaji wa miti kwa kaya
na taasisi za serikali kata ya Visiga ,halmashauri ya Mji wa Kibaha.
Aliitaka jamii wakati
ikipanda miti ya matunda na ya kisasa pia ipande miti ya asili ikiwemo
mninga,mkwaju,mkongo ambayo ina faida zake katika kukuza uchumi pamoja
na kuleta hewa safi .
Sago alifafanua, kwa
mwaka huu wameotesha miche ya miti ya asili ipatayo 13,000 ambayo
wanaisambaza iweze kupandwa taasisi za umma ikiwemo mashuleni ,kwa
wananchi kata ya Visiga miche mitatu mitatu kwa kila kaya na kisha ngazi
ya halmashauri .
“Mpango kazi huu
tulianza miaka mitatu sasa ,katika kata hii,tulianzia taasisi za umma
ikiwemo shule mbalimbali na jamii ili kuwa na uelewa wa kujua faida za
miti hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vinavyokuja” alisisitiza Sago.
Hata hivyo, alieleza,
mpango kazi na mkakati uliopo kwa mwaka 2020 ni kuotesha miti 30,000 na
kuigawa katika kaya na taasisi hizo.
Nae diwani wa kata ya
Visiga Kambi Legeza aliishukuru SAHO kwa kuunga mkono juhudi za
serikali ,”:’na kuelezea hali ya mazingira ni mbaya ,kwakuwa miti
mikubwa inakatwa ovyo kwa ajili ya mkaa ,mbao hali inayosababisha
kutoweka kwa miti ya asili.
Legeza alibainisha ,jitihada iliyopo kwa halmashauri hiyo ,ni kurejesha miti hiyo na kukemea uharibifu wa mazingira.
Kwa upande
wake,Shabani Mchora kutokea Mchangani Visiga, alisema juhudi za shirika
la SAHO zitasaidia kuweka mazingira bora na kuwapa wananchi uelewa wa
kutunza mazingira.
No comments :
Post a Comment