Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas akisalimiana na
wakufunzi wa askari wa Kikosi Maalum kitakachosimamia Ulinzi wa Amani katika Mpaka
wa Tanzania na Msumbiji huko mkoani Mtwara katika Mto Ruvuma ambapo kumekuwa
kukitokea mauaji ya mara kwa mara kwa raia wema yaliosababishwa na wahalifu
kutoka Nchini jirani ya Msumbiji.
Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas akiongea na
askari wanaohitimu mafunzo ya usimamizi
wa Ulinzi katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji yaliofanyika katika pori la West
Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro.
Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas akimkabidhi
cheti cha ukufunzi bora Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP William Mwampagale wakati
akifunga mafunzo ya askari wa Ulinzi wa Amani Kimataifa Kilelepori mkoani Kilimanjaro.
Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la polisi, CP Liberatus Sabas akisalimiana na
wakufunzi wa Askari wa Kikosi Maalum kinachotarajiwa kujiunga na vikosi vingine
vya Ulinzi wa Amani Kimataifa kwaajili ya kusimamia amani katika nchi au
mataifa yenye migogoro.
Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas wa tatu kutoka
kushoto kwa waliokaa akiwa katika picha ya pamoja Maafisa wa Jeshi la Polisi,
wakufunzi wa ndani pamoja na wakufunzi wa umoja wa kimataifa baada ya kufunga
mafunzo Kilelepori mkoani kilimanjaro.
(PICHA
NA JESHI LA POLISI)
No comments :
Post a Comment