Monday, November 18, 2019

WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI (BRELA)YASHIRIKI MAFUNZO YA HATAZA NCHINI MISRI



Tanzania ikiwa kama mwanachama wa Shirika la Miliki Bunifu Duniani (World Intellectual Property-WIPO) Kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) iliyopo chini ya
Wizara ya Viwanda na Biashara Inashiriki Mafunzo ya Hataza kwa Nchi za Africa (Training Course on Patent Search and Examination for African Countries) Nchini Misri kuanzia tarehe 17/11/2019 hadi 21/11/2019
Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Shirika la Miliki Bunifu Duniani (WIPO), Nchi ya Misri na Ofisi ya Hataza ya Misri na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka Nchi 15 za Africa Tanzania imewakilishwa na Bi Suzana Senso-Afisa Mwandamizi Kutoka kitengo cha Miliki Bunifu-Brela
Mafunzo haya yanamanufaa kwa Taifa letu kwenye maswala ya uvumbuzi ili kuweza kuendana na kauli mbiu ya Serikali ya Viwanda
Vumbuzi zinahitajika ili kuwa na Bidhaa na huduma zenye ubora na zenye kukidhi mahitaji ya wananchi,ili kuendana na ulimwengu wa sasa wa Technolojia

No comments :

Post a Comment