
Naibu Katibu mkuu wa wizara ya
maji Mhandisi Anthony Sanga akitoa hutoba yake leo kwenye Ufunguzi wa
warsha ya siku tatu ya mamlaka za maji mikoa inayoendelea jijini Arusha
ambapo amezitaka mamlaka hizo kutumia mafunzo hayo kuleta tija ya
kuondoa uhaba wa maji nchini na kwa kujindesha badala ya kugemea ruzuku
ya serikali

Afisa mtendaji mkuu wa kiwanda cha
kutengeneza mabomba ya plastiki ya maji Plasco Limited ya Dar es salaam
akiongea na vyombo vya habari kwenye warsha ya siku tatu ya masuala ya
jinsi ya kupata fedha za miradi midogo na mikubwa ya maji na kuwataka
wadau hao kutumia fedha zao kidogo wanazokopa kununua biadhaa za hapa
nchini

Sehemu ya maonyesho yaliombatana
na warsha hiyo pichani ni mabomba ya maji yanayotengenezwa na Kampuni za
kitanzania ya Plasco Ltd ya Dar es salaam kama yanavyoonekana
Pichani picha na Ahmed Mahmoud Arusha
……………………….
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wizara ya maji imezitaka mamlaka na wadau wa maji nchini kuhakikisha wanatumia
ushirikiano na uzoefu wao kupata fedha na mikopo
ya kujenga miradi ambayo itatoa huduma bora za maji kwa wananchi na
kuacha tabia ya kuweka taarifa kwenye mafaili.Wizara ya maji imezitaka mamlaka na wadau wa maji nchini kuhakikisha wanatumia
Agizo hilo limetolewa na Naibu
Katibu mkuu wa wizara ya maji Mhandisi Anthony Sanga wakati akifungua
warsha ya siku tatu ya wadau wa maji kutoka mamlaka za maji nchini
iliyoandaliwa na shirikisho la wasambazaji wa maji nchini (Atawas)
jijini Arusha.
Alisema kuwa lengo kubwa la
mafunzo ni upatikanaji wa fedha za miradi ya maji itakayowasaidia
wananchi kupata huduma bora za maji safi na salama kwa bei nafuu kwa
kuwatumia wadau wa taasisi za kifedha kupata mikopo ya ujenzi wa miradi
midogo na mikubwa.
“Wakitoka hapa washiriki wote
wahakikishe wanaenda kutekeleza kwa vitendo ili wananchi wapate huduma
bora za maji za bei nafuu sio kwenda na kuandika taarifa ziishie kwenye
mafaili tunataka utekelezaji wenye tija kwa maendeleo ya tasnia ya maji
nchini”alisisitiza Sanga.
Alieleza kuwa serikali ya awamu ya
tano imejikita kuhakikisha inamtua mama ndoo kichwani hivyo kuwataka
watendaji wote ndani ya wizara hiyo ziwemo mamlaka za maji mikoa
kufanyakazi ya kutekeleza miradi kwa ubora kwa lengo la wananchi kupata
huduma bora za maji ili kufanikisha azma hiyo ya serikali
Kwa Upande wake Mkurugenzi
Mwendeshaji wa kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji ya plastiki
(PLASCO LTD)Allimiya Osman alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikizalisha
mabomba ya maji yenye uwezo mkubwa duniani katika kuhimili, kuhifadhi na
kupitisha maji kwa muda wa mrefu bila kuharibika.
Alisema teknolojia inayotumika
kutengeneza mabomba hayo inatumika kote duniani hivyo kuwataka wadau wa
maji nchini kuhakikisha wanashirikiana na wadau hao wa maji katika
kukambiliana na changamoto za maji katika kuboresha huduma za maji
nchini.
Alisema kuwa ili kufanikiasha
suala zima la utoaji huduma wanasisitiza serikali na wadau wa maji
kuangalia matumizi ya fedha wanazopata kwa kununua bidhaa za viwanda vya
hapa nchini ili kuongeza wigo wa mapato na kupunguza tatizo la ajira.
Awali akiongea na waandishi wa
habari mkurugenzi mwendeshaji wa taasisi ya wadau wa huduma za maji
nchini (ATAWAS)Costantino Fidelis alisema kuwa uhaba wa maji unatokana
na ukosefu wa fedha za ujenzi wa miradi ya maji ndio maana wameamua
kuwajengea uwezo watendaji wa mamlaka za maji mikoa kupata mafunzo ya
kuombea fedha za miradi kutoka kwenye taasisi za kifedha kutekeleza
upatikanaji wa maji nchini
.
Alisema kuwa hayo ndio yamewafanya kuona umuhimu wa kuendesha warsha hiyo ili kuona miradi ya maji ikitekelezwa na kuondoa uhaba wa maji nchini ikiwemo kwenye suala zima la upatikanaji wa fedha kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani
.
Alisema kuwa hayo ndio yamewafanya kuona umuhimu wa kuendesha warsha hiyo ili kuona miradi ya maji ikitekelezwa na kuondoa uhaba wa maji nchini ikiwemo kwenye suala zima la upatikanaji wa fedha kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani
“Matarajio ni kufungua milango kwa
mamlaka za maji kuwa na fedha za kutosha kutekeleza miradi ya maji
nchini ambayo itasaidia kuondoa uhaba wa maji kwa wananchi wengi zaidi
hivyo kufikia malengo ya serikali” alisema Fidelis
No comments :
Post a Comment