
Na.Alex Sonna,Dodoma
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Serikali
za Mikoa na Tawala za Mitaa (ALAT) Elirehema Kaaya,ametoa pongezi kwa
Asasi za Kiraia nchini (Azaki) kwa kusimamia malengo pamoja na
juhudi
walizijiwekea katika kuwanufaisha wananchi.
Hayo ameyasema wakati wa mkutano
wa majadiliano ya wiki ya AZAKI yanayoendelea jijini Dodoma,amesema kuwa
hakika Azaki zimekuwa zikifanya kazi nzuri na kubwa kwa kutoa Elimu kwa
wananchi pamoja Sekta mbalimbali kwa kuwajengea uwezo.
Bw.Kaaya,amesema kuwa wao kama
ALAT wamekuwa wakifanya kazi katika maeneo mbalimbali huku wakikutana
moja kwa moja na wananchi wamekuwa wakiona juhudi zinazofanywa na
Azaki kwa kuunga mkono kazi zinafanywa na Serikali katika kuleta
maendeleo nchini.
” Sisi ni wadau wakubwa wa Azaki
kwa sababu zinagusa moja kwa moja maisha ya wananchi wetu,jukumu letu ni
kuziunganisha Halmashauri zote 185 na malengo yetu ni kutoa huduma kwa
amesisitiza Bw.Kaaya
Amesema kuwa wamekuwa wakifanya
kazi kwa ushirikiano na AZAKI kweli zimekuwa zikituonesha mchango mkubwa
mno hivyo tumejionea ndani ya miaka mitatu wamechangia Bilioni 236
kwenye uchumi wa Nchi yetu.
Hata hivyo ametoa rai kwa Azaki
hizo kujikita zaidi katika kuwajengea wananchi uwezo wa kujitegemea
kiuchumi, kujenga miundombinu ya elimu, afya na kuwawezesha kujikomboa
kimaisha kupitia miradi mbalimbali wezeshi ya kibiashara.
Amesema Serikali ya awamu ya tano
imeweka sera ambayo Halmashauri zote nchini zinatenga asilimia 10 za
bajeti zao kwa ajili ya makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye
Ulemavu hivyo amezitaka Azaki kujikita zaidi katika kuwajengea uwezo
makundi hayo ili waweze kufaidika na mikopo hiyo.
” Mimi napenda kuona matokeo, Watu
wetu wa kijijini anapenda kuona maji salama, huduma ya afya iliyo bora,
nitoe rai kwa Azaki zetu nchini zijikite katika mambo yanayoonekana,
tujikite katika mambo yanayogusa maisha ya watu wetu, tusiangalie sana
matakwa ya wafadhili wetu bali mahitaji haswa ya wananchi ambao tumeamua
kuwafanyia kazi,” Amesema Kaaya.
No comments :
Post a Comment